• HABARI MPYA

  Tuesday, January 02, 2018

  YANGA YAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI 2O18 YAIPIGA 2-1 MLANDEGE

  Na Salum Vuai, ZANZIBAR
  YANGA SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Mlandege katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Amaan, Zanzibar usiku huu.
  Shujaa wa Yanga leo alikuwa ni kiungo aliyetumika kama mshambuliaji leo, Juma Mahadhi aliyefunga mabao yote mawili kipindi cha kwanza.
  Mahadhi aliye katika msimu wake wa pili Yanga SC tangu asajiliwe kutoka Coastal Union ya Tanga, alifunga bao la kwanza dakika ya sita tu ya mchezo akimalizia pasi ya kiungo Pius Buswita na pili akimalizia krosi ya beki Mwinyi Hajji Mngwali dakika ya 36. 

  Juma Mahadhi akipongezwa na Pius Buswita baada ya kufunga mabao mawili ya Yanga leo 

  Katika mchezo huo, Yanga ilipata pigo kipindi cha kwanza baada ya beki wake, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo akikimbizwa hospitali, nafasi yake ikichukuliwa na mkongwe Nadir Haroub ‘Cannavaro.’ 
  Kipindi cha pili pamoja na Yanga kuingia na mkakati wa kuongeza mabao, walijikuta wakifungwa wao dakika ya pili tu tangu kuanza ka kipindi hicho mfungaji Omar Makame dakika ya 48. 
  Beki wa Yanga, Andrew Vincent Chikupe ‘Dante’ alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 88 pamoja na beki wa mshambuliaji wa Mlandege, Omar Makame baada ya kugombana. 
  Iliwachukua dakika mbili tu Simba kupata bao la kuongoza kupitia kwa beki aliyechezeshwa kwenye nafasi yake ya zamani, kiungo Jamal Mwambeleko aliyemalizia kwa kichwa krosi ya beki wa kushoto, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. 
  Mwenge wakasawazisha bao hilo dakika ya 28 kupitia kwa mshambuliaji wao, Humud Abdulrahman Ali aliyefumua shuti baada ya pasi ya Seif Pima Ame.
  Pamoja na timu zote kufanya mabadiliko kipindi cha pili, lakini kupatikana kwa mabao mengine ilishindikana.
  Katika mchezo uliotangulia leo wa Kundi B, Singida United imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Zimamoto hapo hapo Amaan. Mabao ya Singida yamefungwa na Deus Kaseke dakika ya saba, Dany Usengimana dakika ya 21 na Kigi Makasi dakika ya 81, wakati ya Zimamoto yamefungwa na Ibrahim Hamad Ahmada ‘Hilika’ katika daika ya 39 na 84.
  Kikosi cha Mlandege SC kilikuwa;Masoud Kombo, Adam Hamad, Edwin Charles, Omary Hajji, Abubakar Ali, Abubakar Ame, Omar Makame, Hassan Ramadhani, Mohammed Abdallah, Khamis Abuu na Ali Nikenya.
  Yanga SC; Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy, Mwinyi Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’/Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dk30, Said Juma ‘Makapu’, Yussuf Mhilu/, Papy Tshishimbi, Juma Mahadhi, Pius Buswita na Raphael Daudi/Emmanuel Martin dk847. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI 2O18 YAIPIGA 2-1 MLANDEGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top