• HABARI MPYA

  Thursday, January 04, 2018

  YANGA NA JKU, SIMBA NA JAMHURI KOMBE LA MAPINDUZI LEO ZENJI

  Na Salum Vuai, ZANZIBAR
  MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo mitatu kufanyika Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar, vigogo Simba na Yanga wakirejea kazini.
  Mchezo utakaotangulia utakuwa wa kiporo kati ya Taifa Jan’gombe na Singida United mapema Saa 8:30 mchana
  Mechi ililazimika kuahirishwa jana baada ya dakika 45 tu za kipindi cha kwanza kufuatia mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha Uwanja wa Amaan kujaa maji. Na ilivunjika Singida United wakiwa wanaongoza kwa mabao 3-1.
  Baada ya mchezo huo, mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC watakutana na wababe wao wa kihistoria, JKU Saa 10:30 jioni katika mchezo mwingine wa Kundi B.
  Watani wao, Simba wao watakamilisha mechi za leo kwa kumenyana na Jamhuri katika mchezo wa Kundi A Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan.
  Ikumbukwe katika mechi za kwanza juzi, Simba ililazimishwa sare ya 1-1 na Mwenge na Yanga ilishinda 2-1 dhidi ya Mlandege.
  Mechi nyingine ya jana, URA ya Uganda iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mwenge, bao pekee la mkongwe, Bokota Labama.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA JKU, SIMBA NA JAMHURI KOMBE LA MAPINDUZI LEO ZENJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top