• HABARI MPYA

  Friday, January 05, 2018

  YANGA BANDIKA BANDUA MAPINDUZI, WANAKIPIGA TENA LEO NA TAIFA JANG’OMBE

  Na Salum Vuai, ZANZIBAR
  YANGA SC inaingia katika mchezo wake wa tatu wa Kundi B Kombe la Mapinduzi itakapomenyana na Taifa Jang’ombe Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuanzia Saa 2:15 usiku. 
   Mchezo huo unakuja siku moja tu baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKU jana, bao la dakika ya 90 la beki Hassan Ramadhani Kessy.
  Sifa zimuendee mwenyewe Kessy kwa bao hilo, kwani aliingia na mpira ndani kwa kasi kutokea pembeni akampasia Pius Buswita aliyemsogezea mbele beki huyo kwa pasi ya kisigino akaikuta na kufunga.
  Hassan Ramadhani Kessy alikuwa shujaa wa ushindi wa 1-0 wa Yanga jana Kombe la Mapinduzi

  Kwa ushindi huo mwembamba, Yanga SC inafikisha pointi sita baada ya mechi mbili, ikiwemo ya kwanza waliyoshinda 2-1 dhidi ya Mlandege juzi na ikishinda leo itakuwa imejihakikishia kwenda Nusu Fainali hata kabla ya mechi zake mbili za mwisho dhidi ya Zimamoto FC Januari 7 na Singida United Januari 8.
  Mechi ya kwanza leo itakuwa ni kati ya Mlandege na Singida United Saa 8:30, kabla ya URA kumenyana na Azam FC Saa 10:30 jioni.
  Baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi Jamhuri ya Pemba kwenye mchezo wa Kundi A jana usiku, Simba itarejea Uwanja wa Amaan kesho kumenyana na Azam FC Saa 2:15 usiku.
  Ushindi wa jana uliotokana na mabao ya mabao ya washambuliaji, Nahodha John Raphael Bocco, chipukizi Moses Kitandu na beki Mghana, Asante Kwasi uliifanya Simba ifikishe pointi nne baada ya sare ya 1-1 na Mwenge SC katika mchezo wa kwanza.
  Na baada ya mechi ya kesho dhidi ya Azam FC, Simba watarejea Uwanja wa Amaan Januari 8 kumenyana na URA ya Uganda Saa 10:30 jioni kukamilisha mechi zake za Kundi A.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA BANDIKA BANDUA MAPINDUZI, WANAKIPIGA TENA LEO NA TAIFA JANG’OMBE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top