• HABARI MPYA

    Tuesday, January 02, 2018

    SIMBA, YANGA ZAAMSHA MSISIMKO KOMBE LA MAPINDUZI 2018…MECHI ZOTE LIVE AZAM TV

    Na Salum Vuai, ZANZIBAR
    MSISIMKO wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2018 unatarajiwa kuanza leo wakati timu pendwa, Simba na Yanga za Tanzania Bara zitakapoanza kucheza mechi zake Uwanja wa Amaan, Zanzibar ambazo zote zitaonyeshwa kwenye Televisheni ya Azam TV kupitia chaneli ya Azam Sports 2.
    Washindi wa pili msimu uliopita, Simba wataanza na Mwenge Saa 10:30 jioni wakati Saa 2:15 usiku Yanga watapepetana na Mlandege, mechi ambazo zitatanguliwa na mchezo kati ya Singida United na Zimamoto Saa 8:80 mchana.
    Simba ipo Kundi A pamoja na, Azam, URA ya Uganda, Jamhuri na Mwenge, wakati Yanga ipo Kundi pamoja na Singida United, Zimamoto, Mlandege, JKU na Taifa ya Jan’gombe.
    Simba watarudi uwanjani Januari 4 kumenyana na Jamhuri Saa 2:15 usiku, kabla ya kukutana na Azam Januari 6 na kuhitimisha mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na URA Januari 8, 2018 Saa 10:30 jioni.
    Yanga wao watarudi uwanjani  Januari 4 Saa 10:30 jioni kumenyana na JKU, kabla ya kupepetana na Taifa ya Jan’gombe  Saa 2:15 usiku Januari 5, Zimamoto Saa 2:15 usiku Januari 7 na kukamilisha mechi zake za Kundi B Januari 8 kwa kumenyana na Singida United.
    Mabingwa watetezi Kombe la Mapinduzi, Azam FC walianza vizuri michuano kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Mwenge juzi usiku Uwanja wa Amaan.
    Azam watarudi tena uwanjani Januari 3, 2018 kumenyana na Jamhuri SC Saa 10:30, baadaye URA Januari 5, 2018 Saa 10:30, kabla ya kukutana na Simba Januari 6 Saa 2:15 usiku kukamilisha mechi  zake za Kundi A.
    Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Januari 8, wakati Januari 9 itakuwa mapumziko na Nusu Fainali zitafuatia Januari 10, kabla ya kilele mashindano kwa mchezo mtamu wa fainali Januari 13, ambao utahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi visiwani humo, Dk. Ali Mohammed Shein.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA, YANGA ZAAMSHA MSISIMKO KOMBE LA MAPINDUZI 2018…MECHI ZOTE LIVE AZAM TV Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top