• HABARI MPYA

  Friday, January 05, 2018

  SIMBA SC YAFANYA MAANGAMIZI KOMBE LA MAPINDUZI, YAWAPIGA 3-1 JAMHURI

  Na Mwandishi Wetu, FDAR ES SALAAM
  SIMBA SC imepata ushindi wa kwanza kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa mabao 3-1 Jamhuri ya Pemba katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi usiku wa Alhamisi Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Ikitoka kutoa sare ya 1-1 na Mwenge SC katika mchezo wa kwanza, Simba leo ilikuja juu na ikafanikiwa kwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa 2-0, mabao ya washambuliaji, Nahodha John Raphael Bocco na chipukizi Moses Kitandu.
  Kipindi cha pili, Simba SC iliendelea kutawala mchezo na kufanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na mchezaji mpya, beki Mghana, Asante Kwasi aliyesajiliwa kutoka Lipuli ya Iringa baada ya msimu uliopita kuitumikia Mbao FC ya Kwanza ambaye alifunga bao hilo hil dakika ya 58.
  Jamhuri wakafanikiwa kupata bao la kufutia machzoi dakika ya 87 kupitia kwa mshambuliaji wao, Moses Nassro.
  Baada ya mchezo hyo, jopo la Makocha limemchagua mchezaji wa Simba SC koungo, Mwinyi Kazimoto Mwitula kuwa Man of the match baada ya kazi nzuri leo.
  Kikosi cha Jamhuri kilikuwa; Ali Suleiman Mrisho, Mohammed Mgau Mwalimu, Mohammd Omar Said, Mohammed Juma Mohammed, Yussuf Makame Juma, Greyson Gerard Gwalala, Mussa Ali Mbarouk, Abdulatif Omar Mbarouk, Khamis Abrahman Ahmad, Mwalimu Mohammed Khalfan na Ahmed Ali Omar.
  Simba SC; Emmanuel Mseja, Erasto Nyoni, Shiza Nyoni, Juuko Murshid, Asante Kwasi, James Kotei, Nicholas Gyan, Muzamil Yassin, Moses Kitandu, John Bocco na Mwinyi Kazimoto.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAFANYA MAANGAMIZI KOMBE LA MAPINDUZI, YAWAPIGA 3-1 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top