• HABARI MPYA

    Saturday, January 06, 2018

    SAMATTA AANZA MAZOEZI MAALUM YA KURUDI UWANJANI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa Daktari baada ya kupona maumivu ya goti yaliyomuweka nje kwa miezi miwili.
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana mshambuliaji huyo wa KRC Genk ya Ubelgiji amesema kwa sasa anafanya mazoezi maalum ya kukimbia, kuchezea mpira na ya viungo chini ya uangalizi wa daktari, ikiwa ni hatua ya mwisho kuelekea kurejea uwanjani.
    “Nipo kwenye mazoezi ya mwisho, hatua ya mwisho kabla sijajiunga na timu, nafanya mazoezi chini ya usimamizi wa mtaalamu (Daktari) wa maozezi ya viungo,”amesema Samatta.
    Mbwana Samatta ameanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa Daktari baada ya kupona maumivu ya goti yaliyomuweka nje kwa miezi miwili 

    Mbwana Samatta akifanya mazoezi mepesi peke yake mjini Genk 

    Samatta amekamilisha wiki sita za mapumziko kufuatia kuumia mishipa midogo ya goti lake la mguu wa kulia ambayo ilichanika Novemba 4, mwaka jana akiichezea KRC Genk ikilazimishwa sare ya 0-0 na Lokeren katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
    Samatta aliumia akiichezea mechi ya 70 Genk tangu alipojiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Na katika mechi hizo 70, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA AANZA MAZOEZI MAALUM YA KURUDI UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top