• HABARI MPYA

    Friday, January 05, 2018

    MOHAMED SALAH AWA MWANASOKA BORA AFRIKA 2017

    NYOTA wa Liverpool, Mohamed Salah ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa mwaka 2017.
    Salah, mwenye umri wa miaka 25, alipata pointi 625 katika jopo la wapiga kura linaloundwa na makocha wa timu za taifa na Manahodha pamoja na kikundi maalum cha Waandishi wa Habari.
    CAF imemtangaza Salah mshindi katika sherehebzilizofanyika jana akiwashinda mchezaji mwenzake wa Liverpool, Msenegal Sadio Mane na nyota wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang.

    Rais wa CAF, Ahmad akimkabidhi Mohamed Salah tuzo ya Mwanasoka Bora 
    wa Afrika usiku wa jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA  



    Takwimu za Salah, Mane na Aubameyang na kura zao
    MchezajiMechi Mabao Kura 
    Mohamed Salah 57 36 625 
    Sadio Mane36 16507 
    Pierre-Emerick Aubameyang 51 43 311 
    Mshambuliaji huyo wa Misri aliifungia timu yake ya taifa bao lililowapa tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia, wakati pia amekuwa katika kiwango kizuri kwa Wekundu wa Anfield. 
    Tayari Salah ameifungia mabao 23 Liverpool msimu huu baada ya kujiunga nayo akitokea Roma ya Italia na anashika nafasi ya pili kwa ufungaji Ligi Kuu ya England nyuma ya Harry Kane.  
    Salah anaingia kwenye orodha ndefe ya wachezaji waliowahi kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika akiungana na magwiji kama Didier Drogba, George Weah, Roger Milla na Yaya Toure.
    Anakuwa Mmisri wa pili tu kushinda tuzo hiyo baada ya Mahmoud Al Khatib mwaka 1983.
    "Hizi ni ndoto zilizotimia upande wangu. 2017 ulikuwa mwaka hauwezi kuamini kwa timu ya taifa ya Misri na klabu zangu,"alisema Salah kwenye tuzo hizo. 
    "Kufuzu Kombe la Dunia baada ya miaka 28 na kuwa na msimu mzuri Roma na Liverpool ulikuwa wakati maalum katika historia yangu,".'
    Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp aliwaruhusu wachezaji wake wawili walioingia fainali kusafiri hadi Ghana kuhudhuria tuzo hizo ingawa ana mechi na Everton ya Kombe la FA leo. 
    Salah na Mane walitarajiwa kurejea Liverpool kwa ndege maalum baada ya sherehe hizo jana usiku. 
    Kocha wa Misri, Hector Cooper ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka kwa kwawezesha Mafarao kufuzu Fainali za Kombe la dunia mwakani Urusi. 
    Mohamed Salah (katikati) amewashinda Msenegal Sadio Mane (kushoro) na nyota wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang (kulia)

    ORODHA KAMILI YA WASHINDI WA TUZO
    Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika
    Mohamed Salah (Misri na Liverpool)
    Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Kike 
    Asisat Oshoala (Nigeria na Dalian Quanjian)
    Mchezaji Bora Kijana wa Mwaka
    Patson Daka (Zambia na Liefering)
    Kocha Bora wa Mwaka
    Hector Cuper (Misri)
    Klabu Bora ya Mwaka
    Wydad Athletic Club
    Timu ya Taifa ya Mwaka
    Misri
    Timu ya Taifa ya Wanawake ya Mwaka
    Afrika Kusini
    Gwiji
    Ibrahim Sunday (Ghana)
    Tuzo ya Platinum
    Nana Addo Dankwa Akufo-Addo – Rais wa Ghana
    George Weah – Rais Mteule wa Liberia na Mwanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Ulaya na Afrika
    Kikosi cha wachezaji 11 chaguyo la mashabiki
    Kipa: Aymen Mathlouthi (Tunisia  na Etoile du Sahel)
    Mabeki: Ahmed Fathi (Misri na Al Ahly), Eric Bailly (Ivory Coast na Manchester United), Ali Maaloul (Tunisia  na Al Ahly)
    Viungo: Mohamed Ounnajem (Morocco na Wydad Athletic Club), Karim El Ahmadi (Morocco na Feyenoord), Junior Ajayi (Nigeria na Al Ahly), Achraf Bencharki (Morocco na Wydad Athletic Club)
    Washambuliaji: Khalid Boutaib (Morocco na Yeni Malatyaspor), Mohamed Salah (Misri na Liverpool), Taha Yassine Khenissi (Tunisia na Esperance)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOHAMED SALAH AWA MWANASOKA BORA AFRIKA 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top