• HABARI MPYA

  Tuesday, January 16, 2018

  RWANDA YAIKATALIA NIGERIA CHAN, SARE 0-0 LIBYA YASHINDA 3-0

  TIMU ya taifa ya Rwanda imelazimisha sare ya 0-0 na Nigeria katika mchezo wake wa kwanza wa Kundi C michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN jana mjini Tangiers.
  Matokeo hayo yanamaanisha, Libya inaendelea kuongoza kundi hilo baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Equatorial Guinea mapema katika mchezo uliotangulia jana, mabao ya Saleh Taher mawili na Zakaria Alharash.
  Sifa nyingi zimuendee kipa wa Rwanda, Eric Ndayishimiye aliyeokoa michomo mingi ya hatari na kuizuia kabisa timu ya Afrika Magharibi kushinda jana.
  Ally Niyonzima wa Rwanda (kushoto) akiudhibiti mpira dhidi ya Rabiu Ali wa Nigeria jana
  Kwa ujumla Super Falcons walikuwa bora uwanjani zaidi ya Amavubi wakitawala mchezo kwa gonga safi na kushambulia zaidi, lakini wakashindwa kufanya jambo moja tu, kufunga bao.
  Kiungo Djihad Bizimana, mpwa wa kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima alichaguliwa mchezaji bora wa mechi hiyo na michezo ijayo ya kundi hilo, Amavubi itacheza na Equatorial Guinea na Nigeria itamenyana na Libya Alhamisi.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RWANDA YAIKATALIA NIGERIA CHAN, SARE 0-0 LIBYA YASHINDA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top