• HABARI MPYA

  Tuesday, January 16, 2018

  NEEMA YANGA, KAMPUNI YA MARCON YAMWAGA BILIONI 2 MIAKA MITATU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Yanga leo hii imeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Macron wenye thamani ya Sh. Bilioni 2 kwa ajili ya utengenezaji na uuzaji wa jezi za klabu hiyo.
  Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Yanga, Charse Boniphace Mkwasa amesema kwamba mkataba utakuwa na ongezeko kutokana na makubaliano waliyofikia. Kwa mujibu wa Mkwasa ni kwamba dau litakuwa likiongezeka kulinganana idadi ya mauzo ya jezi za mashabiki.
  Ikumbukwe Desemba mwaka huu, Macron walisaini mkataba na miaka miwili na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa udhamini wa jezi wa timu zote za taifa zikiwemo za vijana na wakubwa kwa wanawake na wanaume wenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 800.

  Katibu Mkuu wa Yanga, Charse Boniphace Mkwasa (katikati) na akisaini mkataba na mwakilishi wa Macron (kulia)

  Katika hatua nyingine, Ofisa Habari wa Yanga, Dissmas Ten amesema kikosi kipo tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC utakaoanza Saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Hata hivyo, Ten amesema klabu itaendelea kuwakosa Wazimbabwe, kiungo Thabani Kamusoko, mshambuliaji Donald Ngoma ambao ni majeruhi pamoja na Geofrey Mwashiuya, wakati Mzambia Obrey Chirwa anatumikia adhabu ya kufungiwa ya mechi tatu hadi sasa akiwa amekwishakosa mechi moja.
  "Tunawachezaji wetu ambao bado ni wagonjwa kuna Ngoma, Mwashiuya na Kamusoko wataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Mwadui pamoja na Chirwa ambaye anaitumikia adhabu iliyotolewa na Kamati ya Maadili,” amesema Ten.
  Kuhusu, Mrundi Amissi Tambwe aliyekuwa anasumbuliwa na Malaria, Ten amesema kwamba amepona, lakini kujumuishwa kwenye mchezo wa kesho ni mipango ya mwalimu.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEEMA YANGA, KAMPUNI YA MARCON YAMWAGA BILIONI 2 MIAKA MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top