• HABARI MPYA

    Monday, January 01, 2018

    MVUA YALAZA PAMBANO LA MBEYA CITY NA KAGERA, NONGA AING’ARISHA MWADUI

    Na Mwandishi Wetu, MBEYA
    MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Mbeya City na Kagera Sugar umeshindwa kufanyika mjini Mbeya kutokana na mvua kubwa iliyonyesha leo na Uwanja wa Sokoine kujaa maji.
    Timu zote zilifika uwanjani kwa ajili ya mchezo huo baada ya kikao cha kabla ya mchezo leo asubuhi, lakini kutokana na Uwanja wa Sokoine kujaa maji kwenye eneo la kuchezea, mechi hiyo imeahirishwa hadi keshso saa 10:00 jioni.
    Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, wenyeji Mwadui FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga.
    Paul Nonga amefungwa mabao yote ya Mwadui FC leo ikiilaza 2-1 Ruvu Shooting 

    Mabao ya Mwadui leo yamefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Mbeya City na Yanga SC, Paul Nonga yote wakati la Ruvu limefungwa na Adam Ibrahim.
    Mechi za leo zilitarajiwa kukamilisha raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom tayari kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi na raundi ya tatu ya Azam Sports Federatiojn Cup (ASFC) itakayochezwa kati ya Januari 5 na 7 mwaka huu kabla ya kuingia raundi ya 13 itakayofanyika kati ya Januari 13 na 17, 2018.
    Maana yake, mzunguko wa 12 utakamilishwa kesho kwa mchezo wa kiporo kati ya Mbeya City na Kagera Sugar.  
    Loading...
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MVUA YALAZA PAMBANO LA MBEYA CITY NA KAGERA, NONGA AING’ARISHA MWADUI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

    PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

    Scroll to Top