• HABARI MPYA

  Wednesday, January 03, 2018

  MKONGWE HENRY JOSEPEH AREJEA KUONGEZA NGUVU MTIBWA SUGAR

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIUNGO mkongwe nchini, Henry Joseph Shindika ameanza mazoezi na klabu yake, Mtibwa Sugar baada ta kupona maumivu ya goti yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu.
  Katibu Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabur ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Shindika ameanza mazoezi jana baada ya kukosekana kwa miezi kadhaa.  
  Swabur amesema mchezaji huyo wa zamani wa Simba SC na Kongsvinger ya Norway, amepona kikamilifu baada ya matibabu mazuri aliyopatiwa.
  Aidha, Swabur amesema wachezaji ambao wanakosekana kwa sasa Mtibwa ni wanne tu, ambao ni beki Salum Kanoni, kiungo Mohammed Issa ‘Banka’, washambuliaji Kevin Sabato ambao ni majeruhi wanaokaribia kurudi uwanjani na Stahmil Mbonde ambaye ana ruhusa ya matatizo ya kifamilia.
  Henry Joseph ameanza mazoezi Mtibwa Sugar baada ya kupona maumivu ya goti  

  “Mbonde anaweza kurudi kambini wakati wowote, na hata hawa majeruhi watatu nao maendeleo yao ni mazuri, ni watu ambao tunawatarajia kurudi wakati wowote,”amesema Swabur. 
  Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mara mbili mfululizo 1999 na 2000 wanaendelea na mazoezi katika Uwanja wao wa nyumabani, Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro chini ya kocha wao mkuu, Zuberi Katwila wakati huu ligi imesimama kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.
  Wana Tam Tam hao kwa sasa wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 21, sawa na mabingwa watetezi, Yanga SC – na kwa pamoja wanazidiwa pointi mbili na Singida United walio nafasi ya tatu na pointi tano na Simba na Azam FC zilizoju juuu.
  Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu, Mtibwa Sugar itateremka tena dimbani Januari 13 kumenyana na wenyeji, Lipuli Uwanja wa Samora mkoani Iringa.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKONGWE HENRY JOSEPEH AREJEA KUONGEZA NGUVU MTIBWA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top