• HABARI MPYA

  Thursday, January 11, 2018

  MAN UNITED WATOA PAUNI MILIONI 25 KUMNUNUA SANCHEZ

  KALBU ya Manchester United imeiingilia Manchester City kwenye mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Chile, Alexis Sanchez.
  City imeipa ofa Arsenal ya Pauni Milioni 20 kumtaka Mchile huyo ambaye anataka kuungana tena na kocha Pep Guardiola, lakini United wanajiandaa kupeleka dau karibu na wanalotaka Arsenal, Pauni Milioni 35, wakati kuna mijadala inayoshawishi kiungo Henrikh Mkhitaryan awe sehemu ya mpango huo.
  Inafahamika ofa ya United inaweza kuwa Pauni Milioni 25, huku Jose Mourinho akitarajia kuwapiku mahasimu wake wa nyumbani.

  Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez alikuwa anaelekea kujiunga na Man City - lakini sasa United wameingilia PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Sanchez na wawakilishi wake inaaminika wamekwishakubaliana vipengele binafsi na Man City ikiwemo mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki, lakini United  wanaweza kuwapiku.
  Zote United na City zilijaribu kumsajili Sanchez wakati akijiunga na Barcelona kutoka Udinese ya Italia mwaka 2011 na tena wakati anachagua kujiunga na Arsenal kutoka Barcelona mwaka 2014.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED WATOA PAUNI MILIONI 25 KUMNUNUA SANCHEZ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top