• HABARI MPYA

  Tuesday, January 09, 2018

  MAN UNITED WAPEWA TIMU YA MCHANGANI KOMBE LA FA

  Kocha Jose Mourinho wa Manchester United amepangiwa Yeovil katika raundi ya Nne ya kombe la FA England PICHA ZADII GONGA HAPA  

  RATIBA RAUNDI YA NNE KOMBE LA FA ENGLAND 

  Liverpool vs West Brom
  Peterborough vs Fleetwood au Leicester
  Huddersfield vs Birmingham
  Notts County vs Wolves au Swansea
  Yeovil vs Manchester United
  Carlisle au Sheffield Wednesday vs Stevenage au Reading
  Cardiff au Mansfield vs Manchester City
  MK Dons vs Coventry
  Millwall vs Rochdale
  Southampton vs Watford
  Middlesbrough vs Brighton
  Bournemouth au Wigan vs Shrewsbury au West Ham
  Hull vs Nottingham Forest
  Newport County vs Tottenham
  Norwich au Chelsea vs Newcastle
  Sheffield United vs Preston  
  TIMU ya Manchester United imepangwa na timu ya kiwango cha chini katika Raundi ya Nne ya Kombe la FA, Yeovil Town ya Daraja la Pili, mechi ambayo itachezwa kabla ya mchezo wa kiporo wa Raundi ya Tatu kati ya Brighton na Crystal Palace Uwanja wa AMEX.
  The Glovers, waliyoitoa Bradford kwenye raundi iliyopita wamejikuta wanaangukia kwa timu ya kocha Jose Mourinho Raundi hii.
  Yeovil watawakaribisha vigogo wa England, walioitoa Derby kwenye raundi iliyopita Uwanja wa mashabiki 9,665 wa Huish Park mwishoni mwa mwezi uliopita.
  Tottenham imepangwa na timu ya Daraja la Pili pia na watasafiri kwenda Rodney Parade kucheza na Newport.
  Kikosi cha Mike Flynn kiliwafunga Leeds katika mechi ya aina yake ya Raundi ya Tatu iliyoshuhudiwa Shawn McCoulsky akiifungia bao la ushindi dakkika ya 89 klabu Wales na kuisogeza mbele. 
  Washindi mara saba, Liverpool wamepangiwa West Brom katika mechi nyingine ya timu za Ligi Kuu tupu.
  Chelsea inaweza kukutana na Newcastle, lakini kikosi cha Antonio Conte kwanza lazima kiwatoe Norwich — katika mechi ya marudio baada ya kulazimishwa sare Uwanja wa Carrow Road wikiendi iliyopita.
  Bournemouth nao wanaweza kukutana na West Ham katika mechi ya timu za Ligi Kuu tupu, lakini lazima timu zote zishinde dhidi ya Wigan na Shrewsbury.
  Vinara wa Ligi Kuu, Manchester City wanakabiliwa na safari ya aidha Cardiff au Mansfield na Leicester lazima wafuzu katika mechi ya marudio Fleetwood ili wakamenyana na Peterborough Uwanja wa ABAX.
  Nottingham Forest, waliowatoa mabingwa wa sasa, Arsenal kwa mabao 4-2 Uwanja wa City Jumapili iliyopita, itasafiri kuwafuata wababe wa Championship, Hull baada ya mafanikio hayo. 
  Mechi zote za za Raundi ya nne zitachezwa wikiendi ya Januari 26 na 29.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED WAPEWA TIMU YA MCHANGANI KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top