• HABARI MPYA

  Wednesday, January 17, 2018

  KONGO YAIPIGA 1-0 CAMEROON, MOROCCO UWANJANI LEO CHAN

  BAO pekee la Junior Makiesse dakika ya 73 limeipa ushindi wa 1-0 Kongo dhidi ya Cameroon katika mchezo wa Kundi D michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao mjini Agadir jana.
  Simba Wasiofungika walio chini ya kocha, gwiji wa Cameroon, Rigobert Song walitawala mchezo, lakini wakashindwa kutawala mahesabu ingawa walitengeneza nafasi kadhaa.
  Patrick Moukoko wa Cameroon alikosa bao dakika tatu kabla ya mapumziko akiwa umbali wa mita sita baada ya shambulizi zuri kutoka upande wa kulia ambako Thomas Bawak na Junior Awono waligongeana vizuri.
  Kongo sasa inapanda kileleni mwa Kundi D, baada ya Angola na Burkina Faso kumaliza mechi yao kwa sare ya 0-0 jana jioni.
  CHAN inaendelea leo kwa mechi za Kundi A; wenyeji, Morocco wakimenyana na Guinea Saa 1:30 usiku, kabla ya Sudan kuvaana na Mauritania Saa 4: 30 usiku.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KONGO YAIPIGA 1-0 CAMEROON, MOROCCO UWANJANI LEO CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top