• HABARI MPYA

  Friday, January 12, 2018

  KANE AFIKIA REKODI YA STEVEN GERRARD KUTWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU ENGLAND

  MSHAMBULIAJI Harry Kane amesawazisha rekodi ya gwiji Steven Gerrard kutwaa tuzo sita za Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya England baada ya kushinda na ya mwezi Desemba mwaka 2017.
  Mchezaji huyo wa Tottenham amefunga mabao nane katika mechi sita, zikiwemo hat-tricks mbili mfululizo dhidi ya Burnley na Southampton katika mwezi wa mavuno.
  Ameweka rekodi ya kufunga mabao 39 katika Ligi Kuu kwa mwaka na sasa anaungana na Nahodha wa zamani wa Liverpool katika vitabu vya historia.
  Kane amesema kwamba alifurahi kupata tuzo hiyo wakati akijiandaa kurejea kwenye ligi kwa mchezo wa nyumbani kati ya Spurs na Everton wikiendi hii. 
  Harry Kane akionyesha tuzo yake Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Gerrard alishinda tuzo ya kwanza ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu Machi 2001 na ya mwisho akatwaa miaka 13 baadaye.
  Kane ameongoza katika orodha iliyokuwa na beki wa pembeni wa Chelsea, Marcos Alonso, Marko Arnautovic wa West Ham United, wachezaji wawili wa Liverpool, Roberto Firmino na Mohamed Salah, Jesse Lingard wa Manchester United, Riyad Mahrez wa Leicester City na beki wa Manchester City, Nicolas Otamendi. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KANE AFIKIA REKODI YA STEVEN GERRARD KUTWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top