• HABARI MPYA

  Friday, January 12, 2018

  KADO AONGOZA KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR KUIVAA LIPULI KESHO

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA
  KIPA mkongwe, Shaaban Hassan Kado ni miongoni mwa wachezaji waliowasili na kikosi cha Mtibwa Sugar mjini Iringa leo tayari kwa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Lipuli Uwanja wa Samora kesho.
  Kado amekuwa nje ya kikosi cha Wakata Miwa hao baada ya kuumia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba mwezi Agosti mwajka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na sasa anarejea Ligi Kuu ikikaribia kukamilisha mzunguko wake wa kwanza.
  Pamoja na Kado, mchezaji mwingine mkongwe aliyekuwa majeruhi pia, Henry Joseph Shindika naye yumo kwenye kikosi hicho.
  Shaaban Kado ni miongoni mwa wachezaji wa Mtibwa Sugar waliowasili Iringa leo kuivaa Lipuli kesho

  Kwa ujumla kikosi cha Mtibwa Sugar kilichowasili leo Iringa kinaundwa na makipa Shaaban Kado na Benedictor Tinocco, mabeki Rodgers Gabriel, Hassan Mganga 'Timbe',  Dickson Job, Dickson Daudi, Hassan Isihaka, Cassian Ponera 'Pepe' na Hussein Idd Hante.
  Viungo ni Shaaban Mussa Nditi, Ally Makarani, Ismail Idan 'Chomeka', Saleh Khamis Abdallah, Hassan Dilunga, Mohamed Issa 'Banka' na Henry Joseph Shindika wakati washambuliaji ni Hussein Javu, Riffat Khamis Msuya, Salum Kihimbwa na Haruna Chanongo.
  Baada ya mazoezi ya kutosha katika kambi yao Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro chini ya kocha wao, Zuberi Katwila, Mtibwa Sugar wanataka kuwazima Lipuli kwao.
  Kwa sasa Mtibwa Sugar inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zaake 21 baada ya michezo 12, wakati Lipuli yenye pointi 14 baada ya michezo 12 pia ni ya nane kwenye ligi ya timu 16.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KADO AONGOZA KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR KUIVAA LIPULI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top