• HABARI MPYA

  Friday, January 12, 2018

  GUARDIOLA AWEKA REKODI MPYA LIGI KUU ENGLAND

  Pep Guardiola ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi wa Desemba wa Ligi Kuu ya England kwa mara ya nne mfululizo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  REKODI ZA GUARDIOLA LIGI KUU YA ENGLAND 

  Kutwa Tuzo nyingi mfululizo za Kocha Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya England - 
  Kushinda mechi nyingi mfululizo za Ligi Kuu - 18 
  Matokeo mazuri zaidi katika msimu wa Ligi Kuu - Pointi 62 katika mechi 22  
  Kuelekea kumaliza msimu huu na mabao mengi zaidi katika historia ya LK - 110 
  Kuelekea kumaliza msimu huu na pointi nyingi zaidi katika historia ya LK - 107 
  MSPANIOLA Pep Guardiola ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi wa Desemba wa Ligi Kuu ya England na kuweka rekodi ya kuwa mtu wa kwanza kushinda tuzo hiyo mara nne mfululizo. 
  Manchester City imeshinda mechi sita na sare moja katika mechi zake saba ilizocheza bila kupoteza mwezi uliopita, ikifunga mabao 19 na kufungwa matatu tu. 
  Guardiola ameshinda tuzo hiyo Septemba, Oktoba, Novemba na sasa Desemba huku City ikipoteza pointi nne tu msimu mzima wa ligi.
  City imefurahia ushindi dhidi ya Tottenham, West Ham, Bournemouth, Newcastle, Swansea na Manchester United kabla ya sare ya 0-0 na Crystal Palace katika siku ya mwaka mpya. 
  Vijana wa Guardiola wamefunga mabao manne katika mechi tatu dhidi ya Swansea, Tottenham na Bournemouth - na kuwafunga wapinzani wao wa Jiji, Manchester United 2-1 Uwanja wa Old Trafford Desemba.  
  City sasa inagongoza Ligi Kuu ya England kwa pointi 15 zaidi ya United katika msimu wa pili wa Guardiola nchini England.
  City ambao hawajapoteza mechi msimu huu hadi sasa, wametoa sare na Palace na Everton na katika ubora wao, wamevunja rekodi ya ushindi wa mechi mfululizo baada ya kushinda mechi 18 za Ligi Kuu.
  Mwezi uliopita, Guardiola alimfikia kocha wa Chelsea, Mtaliano Antonio Conte kwa kutwaa tuzo hiyo mara tatu na sasa anampiku kwa tuzo ya nne.  
  Conte alishinda tuzo hiyo kuanzia Oktoba hadi December mwaka 2016 wakati The Blues wakishinda mechi 13 mfululizo hadi kutwaa ubingwa wa Ligi.    
  Kocha gwiji wa United, Sir Alex Ferguson anaongoza kwa kutwaa tuzo mara nyongi, mara 27 - akifuatiwa na mwalimu wa Arsenal, Arsene Wenger aliyetwaa mara 15.  
  Kocha wa sasa United, Jose Mourinho ameshinda tuzo mara tatu tu licha ya kufanya kazi Ligi Kuu ya England kwa miaka saba. 
  Kwa ujumla katika Ligi msimu huu, City imeshinda mechi 20, sare mbili na hijapoteza mechi kati ya 22 ilizocheza ikifunga mabao 64 na kufungwa 13. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GUARDIOLA AWEKA REKODI MPYA LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top