• HABARI MPYA

  Friday, January 12, 2018

  CONTE ANAJUA AMEKALIA KUTI KAVU CHELSEA

  KOCHA Mtaliano Antonio Conte amekiri kwamba hafahamu kama atabaki Stamford Bridge msimu ujao kama bosi wa Chelsea kutokana na kugoma kuongeza mkataba.
  Mtaliano huyo alishinda taji la Ligi Kuu ya England katika msimu wake wa kwanza uliopita, lakini anaamini historia ya Chelsea inamfanya asitabiri atadumu kwa muda gani kama kocha wa The Blues.  
  Chelsea tayari imeanza kutafuta kocha mpya huku uwezekano wa Conte kuondoka mwishoni mwa msimu ukizidi kuongezeka. 

  Antonio Conte amekiri kwamba hafahamu kama atabaki Stamford Bridge msimu ujao kama bosi wa Chelsea PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Na Conte alikuwa wazi alipoulizwa kama ataendelea kuwa katika viunga vya Stamford Bridge msimu wa 2018-19, akisema kwamba historia ya Chelsea kufukuza makocha haimpi nafasi ya kujua hatima yake.
  Max Allegri wa Juventus na Luis Enrique, aliyeachia ngazi Barcelona mwaka jana, wanapewa nafasi kubwa ya kuchunua nafasi yake. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CONTE ANAJUA AMEKALIA KUTI KAVU CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top