• HABARI MPYA

  Friday, January 12, 2018

  BUKAMBU AKARIBIA KUWA MCHEZAJI GHALI ZAIDI AFRIKA

  Cedric Bakambu amekataa ofa za klabu za Ligi Kuu ya England ili ajiunge na Beijing Guoan ya Ligi Kuu ya China kwa dau la rekodi, Pauni Milioni 65 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


  WACHEZAJI GHALI ZAIDI AFRIKA

  1. Cedric Bakambu (Pauni Milioni 65)
  2. Mohamed Salah (Pauni Milioni 39)
  3. Sadio Mane (Pauni Milioni 34) 
  4. Eric Bailly (Pauni Milioni 30)
  5. Islam Slimani (Pauni Milioni 28) 
  MSHAMBULIAJI wa Villarreal, Cedric Bakambu amekataa ofa za klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England ili ajiunge na Beijing Guoan ya Ligi Kuu ya China kwa dau la rekodi, Pauni Milioni 65.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amekubali mkataba wa muda mrefu wa ambao ndani yake atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 307,000 kwa wiki, licha ya nia ya klabub za TottenhamNewcastleWest Brom na West Ham kumtaka.
  Uhamisho huo utakapokamilika, Bakambu atakuwa mchezaji ghali zaidi wa Kiafrika kwa muda wote, akimpiku nyota wa Liverpool, Mohamed Salah aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 39 kutoka Roma.
  Kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita pia anatarajiwa kumpikunSalah atakapokamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 48 kwenda Anfield.
  Lakini hatagharimu zaidi ya Bakambu baada ya klabu ya Beijing Guoan kukubali kutoa Pauni Milioni 35 za uhamisho wake na Milioni 30 nyingine za kodi kwenye chama chao cha soka.
  FA ya China ilitambulisha sheria ya kutisha Mei mwaka jana ili kuzuia wimbi la wachezaji nyota wa kigeni kuingia nchini humo. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BUKAMBU AKARIBIA KUWA MCHEZAJI GHALI ZAIDI AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top