• HABARI MPYA

  Saturday, January 06, 2018

  BOCCO ATHIBITISHWA KUWA NAHODHA MPYA SIMBA SC IKIIVAA AZAM FC LEO USIKU

  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  KAIMU Kocha Mkuu wa Simba SC, Mrundi Masud Juma Irambona leo amemthibitisha mshambuliaji mzoefu, John Raphael Bocco kuwa Nahodha mpya wa timu hiyo, kufuatia kuondoka kwa beki Mzimbabwe, Method Mwanjali.
  Taarifa ya Simba SC iliyotolewa na Mkuu wake wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Hajji Sunday Manara imesema kwamba Bocco atakuwa anasaidiwa na beki wa pembeni, Mohammed Hussein 'Tshabalala' pamoja na kiungo mkongwe, Mwinyi Kazimoto. 
  “Uthibitisho huo umeungwa mkono na uongozi wa klabu na unaamini utaongeza ari zaidi ndani ya timu, sambamba na nidhamu kwenye kikosi chetu,”imesema taarifa ya Manara.
  Na uteuzi huo unafanyika katika siku ambayo Simba itamenyana na timu ya zamani ya Bocco, Azam FC usiku wa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi.
  John Bocco rasmi anakuwa Nahodha mpya wa Simba SC baada ya kuondoka kwa beki Mzimbabwe, Method Mwanjali

  Bocco aliye katika msimu wake wa kwanza Simba tangu ajiunge nayo kutoka Azam FC alikodumu kwa miaka 10 kwa sasa ametokea kuwa kinara wa mabao wa timu hiyo.
  Na dhahiri katika kumuongezea morali azidi kuibeba timu hiyo, kocha Juma aliyejiunga na Simba Oktoba mwaka jana baada ya mafanikio yake katika Ligi Kuu ya Rwanda akiwa na Rayon Sport anampa John uongozi wa timu.    
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOCCO ATHIBITISHWA KUWA NAHODHA MPYA SIMBA SC IKIIVAA AZAM FC LEO USIKU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top