• HABARI MPYA

  Saturday, January 13, 2018

  BINSLUM WAPATA MSIBA

  SHABIKI namba moja wa timu ya Binslum F.C ya Muhimbili, Ramadhani Said ‘Rasco’ (pichani kulia) amefariki dunia alfajiri nyumbani kwao Mtoni, Temeke mjini Dar es Salaam.
  Taarifa ya Binslum F.C. imesema kwamba wamepata pigo kutokana na msiba wa jamaa yao, Rasco ambaye alikuwa alama ya timu yao popote inapocheza.
  “Taratibu za mazishi zitatolewa na familia, msiba upo Temeke. Kwa niaba ya Binslum F.C tunatoa pole kwa familia ya marehemu na Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema,”imesema taarifa ya Binslum F.C.
  Pamoja na kuwa wadhamini na wafadhili na wa timu mbalimbali nchini ikiwemo Mbeya City, lakini Binslum Tyre Limited wanamiliki timu yao, Binslum F.C. ambayo hushiriki mashindano mbalimbali ya maveterani.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BINSLUM WAPATA MSIBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top