• HABARI MPYA

  Wednesday, January 17, 2018

  BABA UBAYA AREJEA KUONGEZA NGUVU MTIBWA SUGAR…SASA BADO MBONDE NA SABATO TU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mtibwa Sugar imeendelea kuimarika kufuatia kurejea kwa beki wake wa kushoto, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ aliyekuwa anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.
  Katibu Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Abubakar Swabur amesema kwamba Baba Ubaya ameungana na kikosi kambini Manungu, Turiani mkoani Morogoro kilichorejea kutoka Iringa ambako mwishoni mwa wiki kilivuna ushindi 1-0 mbele ya wenyeji, Lipuli Uwanja wa Samora, Iringa. 
  Swabur amesema kwamba baada ya kupona kwa Baba Ubaya, ni wachezaji wawili tu ambao wataendelea kukosekana Mtibwa Sugar ambao ni washam uliaji Kelvin Sabato anayesumbuliwa na maumivu ya nyonga na Stahmil Mbonde ambaye yupo kwao, Dar es Salaam kwa matatizo ya kifamilia.

  Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ (kushoto) amerejea mazoezini Mtibwa Sugar baada ya kupona maumivu ya kifundo cha mguu

  Swabur amesema baada ya ushindi wa Iringa, sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Njombe Mji FC utakaopigwa Manungu Complex Jumamosi wiki hii.
  Kwa sasa Mtibwa Sugar inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 24 baada ya kucheza michezo 13 ya Ligi Kuu, ikizidiwa pointi mbili na vinara Simba na Azam FC na yenyewe ikiwazidi kwa pointi tatu, mabingwa watetezi, Yanga SC.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BABA UBAYA AREJEA KUONGEZA NGUVU MTIBWA SUGAR…SASA BADO MBONDE NA SABATO TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top