• HABARI MPYA

  Friday, January 05, 2018

  AZAM YAPIGWA 1-0 NA URA MAPINDUZI, SINGIDA YAENDA NUSU FAINALI

  Na Salum Vuai, ZANZIBAR
  AZAM FC  imeshindwa kuendeleza wimbi la ushindi kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa 1-0 na URA ya Uganda katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Bao pekee lililoizamisha Azam FC iliyokuwa na rekodi ya kutoruhusu nyavu zake kuguswa kwa mechi saba tangu msimu uliopita, limefungwa na Nicholaus Kagaba.
  Katika mchezo huo, Azam FC ilimaliza pungufu baada ya winga wake Mghana, Enock Atta-Agyei kutolewa kwa kadi nyekundu kwa mchezo usio wa kiungwana.
  Mchezo uliotangulia wa Kundi B, Singida United iliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuichapa Mlandege FC 3-0, mabao ya Danny Usengimana kwa penalti, K. Mwambungu na L.Mbia.
  Matokeo hayo yanamaanisha Singida United imetingia Nusu Fainali ya michuano hiyo. Mechi ya mwisho leo inafuatia Saa 2:15 usiku hii kati ya Yanga SC na Taifa ya Jang’ombe.  
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM YAPIGWA 1-0 NA URA MAPINDUZI, SINGIDA YAENDA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top