• HABARI MPYA

  Wednesday, January 10, 2018

  AZAM FC YAFUATA URA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Salum Vuai, ZANZIBAR
  AZAM FC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao 1-0 usiku huu dhidi ya Singida United Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Shaaban Iddi Chilunga aliyefunga dakika ya 78 kwa shuti kali lililompita kama mshale kipa wa Singida, Peter Manyika baada ya kumtoka beki Michael Rusheshangoga upande wa kushoto.
  Azam  FC, ambo ndiyo mabingwa watetezi, sasa watakutana na URA ya Uganda katika fainali Jumamosi hapo hapo Uwanja wa Amaan.
  Shaaban Iddi Chilunga ameifungia Azam FC bao pekee linaloipeleka fainali Kombe la Mapinduzi 2018

  Ikumbukwe katika mchezo uliotangulia leo jioni, URA iliwatupa nje mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
  Na zote, URA na Azam FC zimetokea Kundi A ambako ziliwapiku vigogo, Simba SC ya Dar es Salam walioshindwa kuingia hatua ya mtoano. 
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Razack Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue/Frank Domayo dk46, Joseph Mahundi/Bryson Raphael dk76, Salmin Hoza, Yahya Zayed/Shaaban Iddi dk76, Bernard Arthur/Abdallah Kheri dk82 na Enock Atta Agyei/Iddi Kipagwile dk46.
  Singida United;  Peter Manyika, Michael Rusheshangoga, Shafiq Batambuze, Kennedy Juma, Malik Antiri, Yussuf Kagoma, Deus Kaseke, Lubinda Mundia, Danny Lyanga, Kambale Salita Gentil na Kiggi Makasi/Salum Chuku dk64.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAFUATA URA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top