• HABARI MPYA

    Saturday, January 20, 2018

    MWANZA HAPATOSHI LEO MBAO NA STAND UNITED CCM KIRUMBA

    Na Mwandishi  Wetu, MBEYA   
    LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi tatu zaidi kuchezwa kwenye viwanja tofauti.
    Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Mbao FC wataikaribisha Stand United katika mchezo wa mahasimu wa Kanda ya Ziwa.
    Na Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar wataikaribisha Njombe Mji wakati Mwadui FC wataikaribisha Ndanda FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
    Jumapili kutakuwa na michezo miwili tu, mabingwa watetezi, Yanga SC wakimenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa wakati Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Sokoine.
    Mzunguko wa 14 utakamilishwa Jumatatu kwa mechi mbili, Kagera Sugar wakiikaribisha Simba SC Uwanja wa Kaitaba na Maji Maji wakiwa wenyeji wa Singida United Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
    Wakitoka kulazimishwa sare ya 1-1 na Maji Maji Uwanja wa Maji Maji mjini Songea Alhamisi, Azam FC kesho wanatarajiwa kupigania ushindi ili kuendelea kuwamo kwenye za ubingwa. 
    Mabingwa watetezi, Yanga SC leo watafanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kumenyana na Ruvu Shooting kesho.
    Mechi iliyopita Yanga ililazimishwa sare ambayo haikutarajiwa ya 0-0 na Mwadui FC Uwanja wa Uhuru na sasa inazidiwa pointi saba na vinara, Simba SC baada ya mechi 13.   
    Kikosi cha Simba SC kiliwasili mjini Bukoba kwa ndege jana tayari kwa mchezo wa wake na Kagera Sugar Jumatatu Uwanja wa Kaitaba mjini hmo.
    Simba imeingia Bukoba siku moja tu baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Singida United katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mshambuliaji wake mahiri, Mganda Emmanuel Okwi akifunga mabao mawili.
    Ushindi wa juzi uliifanya Simba SC ifikishe pointi 29, baada ya kucheza mechi 13, ikiwazidi pointi saba mabingwa watetezi, Yanga SC na pointi mbili Azam FC wenye 27 katika nafasi ya pili, wakati Mtibwa Sugar sasa ni ya tatu kwa pointi zae 24 baada ya timu zote kucheza mechi 13.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWANZA HAPATOSHI LEO MBAO NA STAND UNITED CCM KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top