• HABARI MPYA

  Saturday, January 06, 2018

  ARSENE WENGER AFUNGIWA MECHI TATU NA FA YA ENGLAND

  Kocha Arsene Wenger atatumikia adhab ya kukosa mechi tatu England

  KOCHA wa ArsenalArsene Wenger amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Pauni 40,000 kwa kumtolea maneno makali refa kwenye chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo dhidi ya West Bromwich Jumapili iliyopita.Wenger alikasirika baada ya refa Mike Dean kuwazawadia The Baggies penalti ya dakika ya mwisho baada ya mpira uliopigwa na Kieran Gibbs kumfikia mkononi Calum Chambers.
  Alimfuata Dean baada ya mechi na kuanza kumtolea maneno ya kulaumu uamuzi wake baada ya Jay Rodriguez kufunga penalti hiyo kuipatia timu yake sare ya 1-1.
  Wenger alifunguliwa mashitaka na Chama cha Soka England mapema wiki hii na sasa atakosekana kwenye mechi ya Raundi ya Tatu Kombe la dhidi ya Nottingham Forest Jumapili na mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, maarufu kama Carabao dhidi ya Chelsea.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENE WENGER AFUNGIWA MECHI TATU NA FA YA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top