• HABARI MPYA

  Monday, December 11, 2017

  ZANZIBAR HEROES YACHAPWA NA LIBYA 1-0

  Na Mwandishi Wetu, MACHAKOS
  ZANZIBAR imepoteza mchezo wake wa mwisho wa Kundi A Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuchapwa 1-0 na Libya mchana wa leo Uwanja wa Jomo Kenyatta mjini Machakos, Kenya.  
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdoul Karim Twagirumukiza wa Rwanda aliyesaidiwa na Tigle Belachew wa Ethiopia na Herve Kakunze wa Burundi, bao pekee la Libya ambao ni waalikwa kutoka Kaskazini mwa Afrika, limefungwa na Alharaish Zakaria dakika ya 24 kwa shuti la mbali kutoa nje kidogo ya boksi.
  Zanzibar iliyopumzisha baadhi ya nyota wake kwa ajili ya mechi ya Nusu Fainali, ilijitahidi kusaka bao la kusawazisha, lakini bahati haikuwa yao leo.
  Pamoja na kipigo hicho, Zanzibar ya kocha Hemed Suleiman bado inaongoza Kundi A kwa pointi zake saba, kufuatia awali kushinda mechi mbili na sare moja. Libya inapanda hadi nafasi ya pili baada ya ushindi huo, ikifikisha pointi sita baada ya awali kutoa sare za 0-0 mara tatu.
  Wenyeji, Kenya wanahitaji kuifunga Tanzania Bara katika mchezo unaofutia hivi sasa ili kufikisha point inane na kuipiku Libya na kwe nda Nusu Fainali.
  Kikosi cha Zanzibar kilikuwa; Ahmed Ali Suleiman, Mohamed Othman Mmanga, Mwinyi Hajji Mngwali, Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’, Issa Haidari Dau, Abdul-Azizi Makame Hassan, Seif Abdalla Rashid, Abdul-Samad Kassim Ali, Khamis Mussa Makame, Amour Suleiman Muhamad na Adeyum Ahmed Seif/Mohammed Issa ‘Banka’ dk85.
  Libya; Azzaqah Ahmed, Eltribi Ahmed, Elbarasi Taher, Sabbou Motasem, Aleyat Mohamed, Madeen Muhanad, Shafshuf Suhib, Taktak Muftah, Alharaish Zakaria, Almaryami Khalid na Maetouq Ali.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZANZIBAR HEROES YACHAPWA NA LIBYA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top