• HABARI MPYA

    Wednesday, December 13, 2017

    YANGA KUANZIA SHELISHELI LIGI YA MABINGWA, IKITOKA HAPO SAFARI SUDAN AU BOTSWANA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    YANGA itaanza na St Louis ya Shelisheli katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi ya kwanza ikichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na marudiano ugenini. 
    Katika droo iliyofanyika leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu 59 zimepangwa katika Ligi ya Mabingwa na 54 zimo katika Kombe la Shirikisho.
    Mashirikisho ya nchi nane tu hayajawasilisha wawakilishi ambayo ni ya Cape Verde, Chad, Eritrea, Namibia, Reunion, Sao Tome and Principe, Sierra Leone na Somalia.
    Kocha Mzambia wa Yanga, George Lwandamina ataiandaa timu yake kucheza na St Louis ya Shelisheli katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 

    Na ikivuka hatua hiyo, Yanga itakutana na mshindi kati ya Township Rollers ya Botswana na El Merreikh ya Sudan.

    Timu tano hazijapangwa katika hagtua ya awali, ambazo ni Al Ahly ya Misri, mabingwa watetezu, Wydad Casablanca ya Morocco, mabingwa wa Kombe la Shirikisho, TP Mazembe ya DRC, Esperance ya Tunisia na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. RATIBA KAMILI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA KUANZIA SHELISHELI LIGI YA MABINGWA, IKITOKA HAPO SAFARI SUDAN AU BOTSWANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top