• HABARI MPYA

  Wednesday, December 13, 2017

  WYDAD CASABLANCA YATUPWA NJE KOMBE LA DUNIA

  MABINGWA wa Afrika, Wydad Casablanca wameaga michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya kufungwa mabao 3-2 na Urawa Red Diamonds ya Japan katika mchezo wa kuwania nafasi ya tano usiku wa jana Uwanja wa Hazza Bin Zayed mjini Al-'Ayn.
  Mabao ya Wydad ya Morocco yalifungwa na Ismail El Haddad dakika ya 21 na Reda Hajhouj kwa penalti dakika ya 90 na ushei, wakati ya Urawa Red yalifungwa na Maurício dakika ya 18 na 60 na Yosuke Kashiwagi dakika ya 26.
  Wydad ya Morocco iliianza michuano hiyo kwa kuchapwa 1-0 na Pachuca ya Mexico, bao pekee la Victor Alfonso Guzman dakika ya 111 katika mchezo wa Robo Fainali Uwanja wa Zayed Sports City mjini Abu Dhabi.
  Nusu Fainali ya kwanza ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA jana, Gremio ya Brazil iliichapa 1-0 Pachuca ya Mexico, bao pekee la  Everton dakika ya 95 katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 Uwanja wa Hazza bin Zayed mjini Al Ain.
  Mabingwa watetezi, Real Madrid wanaanza kutetea taji laoe kwa kumenyana na Al Jazira usiku wa leo mjini Abu Dhabi, Falme za Kiarabu.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WYDAD CASABLANCA YATUPWA NJE KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top