• HABARI MPYA

  Tuesday, December 12, 2017

  SINGIDA UNITED YAONGEZWA KOMBE LA MAPINDUZI

  Na Hassan Mvulla, DAR ES SALAAM 
  KAMATI ya Maandalizi ya Kombe la Mapinduzi imeongeza Singida United kwenye michuano ambayo hufanyika kila mwaka visiwani Zanzibar.
  Katibu Msaidizi wa Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Mapinduzi, Khamis Shaali Chumu ameiambia Bin Zubeiry Sportys – Online leo kwamba idadi ya timu zitakazoshiriki michuano hiyo 2018 sasa imeongezeka hadi kufika 11. Hata hivyo, Chuumu hakusema Singida itaingizwa kundi gani.
  Ikumbukwe Kundi A linaundwa na timu za Simba, Azam FC, Jamhuri, Taifa ya Jang’ombe na URA ya Uganda, wakati Kundi B lina Yanga, JKU, Mlandege, Zimamoto na Shaba.
  Kwa mujibu wa ratiba, Simba SC itafungua dimba na URA ya Uganda Januari 2, mwaka 2018 Uwanja wa Amaan, Zanzibar mchezo ambao utaanza Saa 2:15 usiku.
  Mahasimu wao, Yanga wataanza na JKU ya Zanzibar Januari 1, Uwanja wa Amaan pia, mchezo ambao nao utaanza Saa 2:15 usiku.
  Mabingwa watetezi, Azam FC wataanza na Jamhuri katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Amaan pia Januari 2, lakini kuanzia Saa 10:15 jioni. 
  Ufunguzi rasmi wa Kombe la Mapinduzi 2018 utafanyika Desemba 30, mwaka huu kwa mechi mbili kuchezwa Uwanja wa Amaan, kwanza Zimamoto na Mlandege Saa 10:17 jioni na baadaye JKU na Shaba Saa 2:15 usiku.        
  Simba itamenyana na Azam FC Januari 6, ikitoka kukipiga na Taifa ya Jang’ombe Januari 4, kabla ya kumalizia mechi zake za Kundi A Januari 8 na Jamhuri.
  Azam FC itacheza na Taifa ya Jang’ombe Januari 4 kuanzia Saa 10:15, kabla ya kumenyana na Simba na itahitimisha mechi zake za Kundi A kwa kuumana na URA Januari 8 Saa 10;15 pia jioni Uwanja wa Amaan.
  Baada ya mechi na JKU, Yanga watarudi tena uwanjani Januari 3 kwa mchezo na Shaba, Januari 5 na Zimamoto kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kumenyana na Mlandege Janauri 7 Uwanja wa Amaan.
  Nusu Fainali zinatarajiwa kuchezwa Januari 10 na Fainali itakuwa Januari 13, mwaka 2018 Uwanja wa Amaan kuanzia Saa 2:15 usiku. Wazi ratiba hiyo itabadilika kidogo baada ya kuongezwa kwa Singida.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED YAONGEZWA KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top