• HABARI MPYA

  Friday, December 08, 2017

  SIMBA SC 'YAIMIMINIA' 3-1 KMC KIRAFIKI CHAMAZI, MZAMBIA SAKUWAHA AFUNGA

  Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
  VINARA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC usiku huu wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi yq timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  KMC inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Freddy Felix Minziro, walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya saba tu ya mchezo huo lililofungwa na Reyman Mgungila kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya 18 baada ya mchezaji wao kuchezewa rafu.
  Bao hilo lilidumu kwa dakika tisa tu kabla ya Simba kusawazidha kwa mkwaju wa penalti wa John Bocco baada ya Mohamed Ibrahim 'Mo' kuangushwa ndani ya penati boksi.

  John Bocco (kulia) amefunga mabao mawili leo Simba ikishinda 3-1 dhidi ya KMC Chamazi

  Simba walicheza kwa spidi huku wakionyesha wazi kulisaka bao kutokana na mipango yao huku wakikosa nafasi kadhaa.
  Lakini juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 39 baada ya kupata bao la pili lililofungwa na Jonas Sakuwaha mchezaji wa kimataifa wa Zambia anayefanya majaribio ndani ya kikosi cha Simba.
  Mabao hao yalidumu hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza kinamalizika huku Wekundu hao wa Msimbazi wakilisakama lango la KMC mara kwa mara.
  Kipindi cha pili kilianza kwa kasi hukuSimba wakionekana kuingia na nguvu mpya na KMC wakifanya mabadiliko ya wachezaji kadhaa.
  Simba waliendeleza mashambulizi kwenye lango la KMC huku Mwinyi Kazimoto, Nemla na Bocco wakipoteza nafasi kadhaa za mabao.
  Kama ni nyota wa mchezao huo basi ilimstahili kiungo Mwinyi Kazimoto kutokana na kazi kubwa aliyokuwa anaifanya.
  Simba waliendeleza mashambulizi kwa KMC na dakika ya 86 John Bocco aliiandikia Simba bao la tatu kwa shuti la mguu wake wa kulia akipokea pasi safi ya krosi iliyopigwa na Jamal Mwambeleko.
  Mchezo huo kwa Simba ulikuwa wa kujipima nguvu baada ya mazoezi ya wiki moja chini ya kocha wake msaidizi Masudi Juma wakijiandaa na mwendelezo wa Ligi Kuu Bara ambayo kwa sasa imesimama kupisha michuano ya Cecafa.
  Kikosi cha Simba; Emmanuel Mseja, Ally Shomari, Jamali Mwambeleko, Paul Bukaba, Yusuph Mlipili, Said Ndemla, Mohamed Ibrahim/ Vicent Coster, Mwinyi Kazimoto, John Bocco, Jonas Sakuhawa na  Juma Luizio/ 17.
  Kikosi cha KMC; Zacharia Mwaluko, Khalfan Mbarouk, Juma Jabu, Oscar Anania,  Augustino Samson, Reyman Mgungila, Karage Mgunda, Abdulhalim Humud, Hassan Mohamed, Nsama Ludovic na Adam Kingwande.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC 'YAIMIMINIA' 3-1 KMC KIRAFIKI CHAMAZI, MZAMBIA SAKUWAHA AFUNGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top