• HABARI MPYA

  Tuesday, December 12, 2017

  SIMBA KUANZA KUTETEA KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION DESEMBA 22 DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC itaanza kutetea Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) kwa kumenyana na Green Warriors, zote za Dar es Salaam Desemba 22 Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Baada ya droo ya michuano hiyo Desemba 6, mwaka huu kwenye Studio za Kituo cha Televisheni cha Azam, kilichopo Tabata relini, Dar es Salaam, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa ratiba rasmi ya mechi hizo za raundi ya pili ambazo zitachezwa kwa siku tano mfululizo kuanzia Desemba 20, 21, 22, 23 na 24. 
  Ratiba hiyo iliyotolewa leo Desemba 12, 2017  inaonesha michezo ya Desemba 20, mwaka huu itakutanisha timu za JKT Mlale na KMC; Toto African ya Mwanza na Eleven Stars ya Kagera; Ambassador na JKT Oljoro; Boma FC na Ndanda; Mvuvumwa na JKT Ruvu; Abajalo itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons wakati Milambo ya Tabora itacheza Buseresere ya Geita. 
  Desemba 21, 2017 Mshikamano itacheza na Polisi Tanzania; Rhino ya Tabora na Alliance ya Mwanza; Majimaji Rangeres ya Lindi itapambana na Mbeya Kwanza ya Mbeya; Njombe Mji na Mji Mkuu ya Dodoma; Ashanti na Friends Rangers za Dar es Salaam; Kagera Sugar na Makambako wakati Stand United ya Shinyanga itacheza na AFC ya Arusha.
  Desemba 22, mwaka huu kutakuwa na mechi za Green Warriors na Simba; Polisi Dar itapambana na Mgambo JKT ya Tanga; Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya Dar ila kwa sasa imeweka maskani Shinyanga; Biashara ya Mara itacheza na Mawenzi Market ya Morogoro; Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani itacheza na Madini FC ya jijini Arusha huku Mufindi United na Pamba ya Mwanza ilihali Singida United itacheza na Bodaboda FC.
  Siku ya Desemba 23, mwaka huu Azam FC itacheza na Area C; African Lyon ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani; Makanyagio itapambana na Mbao; Mwadui na Pepsi; Majimaji na New Generation wakati Mbeya City itacheza na Ihefu.
  Desemba 24, 2017 Yanga watacheza na Reha FC; Burkina ya Morogoro na Lipuli ya Iringa;  Coastal Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma; Shupavu na Real Mojamoja wakati Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA KUANZA KUTETEA KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION DESEMBA 22 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top