• HABARI MPYA

  Thursday, December 14, 2017

  RONALDO AWEKA REKODI MPYA YA MABAO KOMBE LA DUNIA

  Mshambuliaji Mreno, Cristiano Ronaldo akiifungia bao la kusawazisha Real Madrid dakika ya 53, kufuatia Romarinho kutangulia kuifungia Al Jazira dakika ya 41 katika mchezo wa Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA usiku wa jana Uwanja wa Sheikh Zayed Sports City mjini Abu Dhabi, Falme za Kiarabu (UAE). Gareth Bale aliifungia bao la ushindi Real Madrid dakika ya 81 huku Ronaldo akivunja rekodi ya mabao kwenye michuano hiyo kihistoria baada ya kufikisha mabao sita, sasa akiwazidi Lionel Messi, Luis Suerez wote wa Barcelona wenye mabao matano kila mmoja sawa na Cesar Delgado wa Monterrey ya Mexico PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AWEKA REKODI MPYA YA MABAO KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top