• HABARI MPYA

    Sunday, December 03, 2017

    PIGO BARCELONA, UMTITI AUMIA ATAKUWA NJE HADI MWAKANI

    KLABU ya Barcelona imepata pigo baada ya beki wake, Samuel Umtiti kuumia nyama za paja na atatakiwa kuwa nje hadi mwaka mpya, maana yake ataikosa El Clasico dhidi ya mahasimu, Real Madrid.
    Vigogo wa Katalunya walilazimishwa sare ya 2-2 na Celta Vigo Jumamosi Uwanja wa Nou Camp, mabao yao yakifungwa na nyota wake, Lionel Messi na Luis Suarez.
    Lakini vinara hao wa La Liga wakamaliza mchezo huo na pigo zaidi baada ya Umtiti kuumia.
    Umtiti mwenye umri wa miaka 24, alikuwa anamdhibiti mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Iago Aspas wakati anaumia. 

    Barcelona imethibitisha Samuel Umtiti atakuwa nje hadi mwakani baada ya kuumia nyama za paja PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Baada ya mchezo wa jana, Barca ikathibitisha kupitia tovuti yake kwamba habari mbaya kuhusu mchezaji huyo, Umtiti atakuwa nje hadi mwaka 2018.
    "Vipimo vinaonyesha kwamba Samuel Umtiti ameumia nyama za paja mguu wake wa kulia na anatarajiwa kuwa nje kwa wiki nane,"imethibitisha klabu.
    Maana yake mchezaji huyo atakosekana kwenye safari ya Madrid kwenda kuvaana na wenyeji, Real Madrid Desemba 23 na atarejea uwanjani mwishoni mwa Januari.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO BARCELONA, UMTITI AUMIA ATAKUWA NJE HADI MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top