• HABARI MPYA

  Saturday, December 09, 2017

  PHIL JONES FITI KUICHEZEA MAN UNITED DHIDI YA CITY KESHO

  BEKI wa Manchester United, Phil Jones yuko fiti kwa mchezo dhidi ya mahasimu, Manchester City kesho Uwanja wa Old Trafford, lakini Eric Bailly atakosekana na Marouane Fellaini yuko shakani.
  Jones anatarajiwa kucheza mechi ya mahasimu wa Jiji la Manchester baada ya kukosekana kikosini United tangu kipigo cha Chelsea Novemba 5 baada ya kuumia akiichezea England dhidi ya Ujerumani mchezo wa kirafiki.
  Bailly pia aliumia kwenye mchezo wa kimataifa, akiichezea Ivory Coast na hajapona maumivu ya nyonga, lakini Nemanja Matic anacheza licha ya kuwa na maimivu ya misuli.

  Jose Mourinho amesema Phil Jones atakuwa fiti kucheza kesho mechi ya mahasimu wa Jiji la Manchester PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Fellaini amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti na kocha Jose Mourinho anatumai Mbelgiji huyo atakuwa fiti kucheza kwenye mechi dhidi ya majirano wao hao.
  Akizungumzia taarifa za wachezaji wake, Mourinho alisema: "Zlatan (Ibrahimovic) atakuwepo, Jones atakuwepo, Fellaini itanibidi nisubiri hadi kesho. (Michael) Carrick hatakuwepo, Bailly hatakuwepo. Matic ni majeruhi lakini anacheza,". 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PHIL JONES FITI KUICHEZEA MAN UNITED DHIDI YA CITY KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top