• HABARI MPYA

    Friday, December 08, 2017

    NI RONALDO TENA MSHINDI BALLON D'OR KWA MARA YA TANO KAMA MESSI

    Cristiano Ronaldo akiwa ameshika tuzo ya Ballon d'Or baada ya kukabidhiwa leo mjini Paris, Ufaransa PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    10 BORA YA BALLON D'OR 2017

    1. Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
    2. Lionel Messi (Barcelona)
    3. Neymar (PSG)
    4. Gianluigi Buffon (Juventus)
    5. Luka Modric (Real Madrid)
    6. Sergio Ramos (Real Madrid)
    7. Kylian Mbappe (PSG)
    8. N'Golo Kante (Chelsea)
    9. Robert Lewandowski (Bayern)
    10. Harry Kane (Tottenham) 
    MRENO Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, maarufu kama Ballon d'Or mwaka 2017.
    Ronaldo ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya tano katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Eiffel Tower akiwaangusha Muargentina Lionel Messi na Mbrazil Neymar.
    Ronaldo anayechezea Real Madrid sasa analingana na Messi wa Barcelona, zote za Hispania kwa kutwaa mara nyingi zaidi Ballon d'Or, kila mmoja mara tano.
    Na mafanikio yake yanafuatia kuiwezesha Real Madrid kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga msimu uliopita wa 2016-17.
    Mshindi wa 2017 ametajwa kwa mbwembwe za aina yake, akitokea kwenye video ukumbi wa Eiffel Tower na akaonekana Ronaldo amesimama akiwa ameshika tuzo yake.
    "Ndiyo, najisikia furaha. Ni wakati mzuri katika maisha yangu," amesema Ronaldo wakati anakabidhiwa tuzo. Ni kitu fulani natumai kushinda kila mwaka. Nawashukuru wachezaji wenzangu wa Real Madrid. Na ninataka kuwashukuru watu wengine walionisaidia kufikia kiwango bhiki,". 
    Ronaldo mwenye umri wa miaka 32, ambaye baadaye alifuatwa na mama yake, Maria Dolores dos Santos Aveiro na mtoto wake wa kioume mkubwa, Cristiano Ronaldo Jr huku mpenzi wake, Georgina Rodriguez akitazama kutoka eneo la watu.
    Ronaldo ameshinda tuzo hiyo inayoandaliwa nchini Ufaransa baada ya kuwabwaga wachezaji wengine 29 kutokana na kura za kikundi cha Waandishi wa Habari 173.
    Messi ameshika nafasi ya pili, kwa mara ya saba wawili hao wakishika nafasi mbili za mwanzo za Ballon d'Or katika ushindani wao na Neymar amekuwa wa tatu.

    George Weah anabaki kuwa Mwafrika pekee aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 1995 PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


    Orodha kamili ya washindi wa Ballon d'Or tangu 1956:

    1956 Stanley Matthews (Blackpool), 1957 Alfredo Di Stefano (Real Madrid), 1958 Raymond Kopa (Real Madrid), 1959 Alfredo Di Stefano (Real Madrid), 1960 Luis Suarez (Barcelona), 1961 Omar Sivori (Juventus), 1962 Josef Masopust (Dukla Prague), 1963 Lev Yashin (Dynamo Moscow), 1964 Denis Law (Manchester United), 1965 Eusebio (Benfica), 1966 Bobby Charlton (Manchester United), 1967 Florian Albert (Ferencvaros), 1968 George Best (Manchester United), 1969 Gianni Rivera (Milan), 1970 Gerd Muller (Bayern Munich), 1971 Johan Cruyff (Ajax), 1972 Franz Beckenbauer (Bayern Munich), 1973 Johan Cruyff (Barcelona), 1974 Johan Cruyff (Barcelona), 1975 Oleg Blokhin (Dynamo Kiev), 1976 Franz Beckenbauer (Bayern Munich), 1977 Allan Simonsen (Borussia Monchengladbach), 1978 Kevin Keegan (Hamburg), 1979 Kevin Keegan (Hamburg), 1980 Karl-Heinz Rummenigge (Bayern Munich), 1981 Karl-Heinz Rummenigge (Bayern Munich), 1982 Paolo Rossi (Juventus), 1983 Michel Platini (Juventus), 1984 Michel Platini (Juventus), 1985 Michel Platini (Juventus), 1986 Igor Belanov (Dynamo Kiev), 1987 Ruud Gullit (Milan), 1988 Marco van Basten (Milan), 1989 Marco van Basten (Milan), 1990 Lothar Matthaus (Inter Milan), 1991 Jean-Pierre Papin (Marseille), 1992 Marco van Basten (Milan), 1993 Roberto Baggio (Juventus), 1994 Hristo Stoichkov (Barcelona), 1995 George Weah (Milan), 1996 Matthias Sammer (Borussia Dortmund), 1997 Ronaldo (Inter Milan), 1998 Zinedine Zidane (Juventus), 1999 Rivaldo (Barcelona), 2000 Luis Figo (Real Madrid), 2001 Michael Owen (Liverpool), 2002 Ronaldo (Real Madrid), 2003 Pavel Nedved (Juventus), 2004 Andriy Shevchenko (Milan), 2005 Ronaldinho (Barcelona), 2006 Fabio Cannavaro (Real Madrid), 2007 Kaka (Milan), 2008 Cristiano Ronaldo (Manchester United), 2009 Lionel Messi (Barcelona), 2010 Lionel Messi (Barcelona), 2011 Lionel Messi (Barcelona), 2012 Lionel Messi (Barcelona), 2013 Cristiano Ronaldo (Real Madrid), 2014 Cristiano Ronaldo (Real Madrid), 2015 Lionel Messi (Barcelona), 2016 Cristiano Ronaldo (Real Madrid). 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI RONALDO TENA MSHINDI BALLON D'OR KWA MARA YA TANO KAMA MESSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top