• HABARI MPYA

  Sunday, December 10, 2017

  MSHAMBULIAJI MPYA MGHANA, ARTHUR AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO AZAM

  Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
  KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imetoka sare ya bao 1-1 na Friends Ranger katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenue Uwanja wa Azam Complex usiku wa jana.
  Ilikuwa ni siku nzuri kwa mshambuliaji mpya wa timu hiyo Bernard Arthur, aliyekuwa akicheza mechi yake ya kwanza tokea asajiliwe akitokea Liberty Professional ya Ghana baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 68.
  Mpira huoa ulikuwa ni mkali sana ambapo Azam FC ilicheza vema kipindi cha pili baada ya mabadiliko ya kuingia winga Enock Atta, kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Wazir Junior.
  Mshambuliaji mpya Mghana wa Azam, Bernard Arthur akikimbia kushangilia baada ya kufunga 

  Friends Ranger ilijipatia bao lake dakika ya 65 kupitia kwa Mau Gola kufuatia uzembe uliofanyika kwenye safu ya ulinzi ya Azam FC kabla ya dakika tatu baadaye matajiri hao kusawazisha.
  Azam FC iliutumia mchezo huo kama sehemu ya kuwapa ushindani wachezaji wake kutokana na kusimama kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kupisha michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Kenya.
  Kikosi cha Azam FC jana kilikuwa; Mwadini Ally, Swaleh Abdallah, Hamimu Abdallah/Daniel Amoah dk 76, David Mwantika, Agrey Moris/Oscar Masai dk 86, Salmin Hoza, Braison Raphael/Enock Atta dk 66, Masoud Abdallah/Frank Domayo dk 61, Ramadhan Singano/Wazir Junior dk 61, Bernard Arthur/Paul Peter dk 70, Joseph Mahundi
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSHAMBULIAJI MPYA MGHANA, ARTHUR AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top