• HABARI MPYA

  Thursday, December 07, 2017

  MAN CITY WAPOTEZA MECHI YA KWANZA TANGU MWEZI APRILI

  Wachezaji wa Manchester City, kutoka kushoto Ederson, Yaya Toure, Bernardo Silva na Fernandinho wakitembea kinyonge baada ya kushindwa kuendeleza rekodi yao ya kutopoteza mechi tangu Aprili mwaka huu kufuatia kuchapwa mabao 2-1 jana na wenyeji, Shakhtar Donetsk kwenye mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Oblasny Sport Komplex Metalist mjini Kharkiv. Mabao ya Shakhtar Donetsk yalifungwa na Bernard dakika ya 26 na Ismaily dakika ya 32, wakati la Man City lilifungwa na Sergio Aguero kwa penalti dakika ya 90 na ushei. Man City inafuzu kama mshindi wa Kundi F kwa pointi zake 15 ikiungana na washindi wao wa pili, Shakhtar Donetsk waliomaliza na pointi 12 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY WAPOTEZA MECHI YA KWANZA TANGU MWEZI APRILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top