• HABARI MPYA

  Tuesday, December 05, 2017

  KIGOGO ARSENAL AZURU OFISI ZA CAF CAIRO LEO KUWAPA MIPANGO

  MAKAMU Mwenyekiti wa zamani wa vigogo wa Uingereza, Arsenal na Chama cha Soka England (FA), David Dein anatarajiwa kuzuru ofisi za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) leo.
  Dein atazuru makao makuu ya CAF mjini Cairo, Misri leo kuzungumza na wafanyakazi na kubadilishana mawazo juu ya namna ya kuendeleza mchezo wa soka barani.
  akiwa maarufu zaidi kwa nafasi yake Arsenal kati ya mwaka 1983 na 2007, atawasilisha ubunifu wa muundo wa Ligi Kuu, ambayo imekuwa moja ya bidhaa kubwa za kibiashara kwenye ulimwengu wa soka.
  David Dein anatarajiwa kuzuru ofisi za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) leo.Dein ambaye kwa sasa anatumia muda wake mwingi kuzuru kwenye shule na magereza kuhutubia, pia atajadili namna ya kuboresha michuano ya klabu barani ambayo ni Kombe la Shirikisho n Ligi ya Mabingwa.
  Dein amewahi pia kuwa Rais wa Umoja wa Klabu Kubwa Ulaya, G-14 kati ya Oktoba 2006 na Mei 2007 na amekuwa kwenye Kamati mbalimbali za FIFA na UEFA ikiwemo Kamati ya Mashindano ya Klabu ya UEFA.
  Agosti mwaka 2007 aliuza hisa zake Arsenal F.C. kwa mfanyabiashara Mrusi wa London, mmiliki wa Red and White Holdings.
  Alikuwa pia Rais wa kampeni za  England kuwania uenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIGOGO ARSENAL AZURU OFISI ZA CAF CAIRO LEO KUWAPA MIPANGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top