• HABARI MPYA

    Wednesday, December 13, 2017

    JKU YAPEWA ZESCO, ZIMAMOTO NA WAHABESHI…WAKIVUKA HAPO SASA HILO BALAA LAKE!

    Na Salum Vuai, ZANZIBAR
    TIMU ya Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ya Zanzibar itaanza na Zesco United ya Zambia katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
    JKU SC wataanzia nyumbani Uwanja wa Amaan, Zanzibar kabla ya kusafiri hadi Ndola kwa mchezo wa marudiano.
    Katika droo iliyofanyika leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), timu 59 zimepangwa katika Ligi ya Mabingwa na 54 zimo katika Kombe la Shirikisho.
    Mashirikisho ya nchi nane tu hayajawasilisha wawakilishi ambayo ni ya Cape Verde, Chad, Eritrea, Namibia, Reunion, Sao Tome and Principe, Sierra Leone na Somalia.
    JKU ya Zanzibar itaanza na Zesco United ya Zambia katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika

    Na ikivuka hatua hiyo, JKU itakutana na mshindi kati ya mwakilishi wa Benin dhiai ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

    Timu tano hazijapangwa katika hagtua ya awali, ambazo ni Al Ahly ya Misri, mabingwa watetezi, Wydad Casablanca ya Morocco, mabingwa wa Kombe la Shirikisho, TP Mazembe ya DRC, Esperance ya Tunisia na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
    Wawakilishi wa Zanzibar katika  Kombe la Shirikisho Afrika, Zimamoto wao wataanzia nyumbani pia dhidi ya Wolaitta Dicha ya Ethiopia na wakivuka hatua hiyo watakutana na Zamalek ya Misri.
    Timu tano hazijapangwa katika hagtua ya awali, ambazo ni Al Ahly ya Misri, mabingwa watetezu, Wydad Casablanca ya Morocco, mabingwa wa Kombe la Shirikisho, TP Mazembe ya DRC, Esperance ya Tunisia na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKU YAPEWA ZESCO, ZIMAMOTO NA WAHABESHI…WAKIVUKA HAPO SASA HILO BALAA LAKE! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top