• HABARI MPYA

    Monday, December 11, 2017

    BARCA NA CHELSEA, REAL MADRID NA PSG 16 BORA LIGI YA MABINGWA

    Lionel Messi ataiongoza Barcelona dhidi ya Chelsea kuwania tiketi ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


    RATIBA 16 BORA LIGI YA MABINGWA ULAYA 

    Juventus vs Tottenham
    Basle vs Manchester City 
    Porto vs Liverpool
    Sevilla vs Manchester United
    Real Madrid vs Paris Saint-Germain
    Shakhtar Donetsk vs Roma 
    Chelsea vs Barcelona 
    Bayern Munich vs Besiktas  
    (Mechi za kwanza zitachezwa Februari 13/14 na Februari 20/21. Marudiano yatakuwa Machi 6/7 ma Machi 13/14)
    TIMU za Barcelona na zitaendeleza upinzani wao wa muda mrefu kwenye michuano ya Ulaya baada ya kupangwa pamoja katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
    Kikosi cha Antonio Conte kilizidiwa kete kileleni mwa Kundi C na Roma na sasa kitasafiri kwenda Nou Camp kwa mchezo wa mtoano. 
    Tottenham iliyovuna pointi nyingi zaidi kihistoria msimu huu, itamenyana na mabingwa wa Italia, Juventus, waliomaliza nyuma ya Barcelona kwenye Kundi D.
    Vibara wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wamepangiwa timu nafuu kidogo Basle, wakati Liverpool baada ya kuongoza Kundi E itamenyana na Porto.
    Hii inakuwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2003-2004 timu tano kutoka nchi moja kuingia hatua ya mtoano. 
    Timu nyingine ya England katika hatua hii, Manchester United itamenyana na Sevilla ya Hispania kuwania tiketi ya Robo Fainali. 
    Katika droo iliyopangwa leo, mabingwa watetezi, Real Madrid watamenyana na Paris Saint-Germain.
    Chelsea na Barcelona zimekutana mara 15 kwenye michuano ya Ulaya, kila timu ikishinda mechi tano na nyingine tano zimetoka sare. 
    Mechi za kwanza za 16b Bora zitachezwa Februari 13 na 14 na Februari 20 na 21, wakati marudiano yatakuwa Machi 6 na 7 na Machi 13 na 14.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCA NA CHELSEA, REAL MADRID NA PSG 16 BORA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top