• HABARI MPYA

  Monday, December 11, 2017

  ARSENAL YAPELEKWA SWEDEN 32 BORA EUROPA LEAGUE

  TIMU ya Arsenal itamenyana na Ostersunds ya Sweden inayomilikiwa na Muingereza, Graham Potter katika hatua ya 32 ya Europa League.
  Atletico Madrid imepangwa na Copenhagen wakati Borussia Dortmund itamenyana na Atalanta, iliyoifunga Everton nyumbani na ugenini na kuongoza Kundi E.
  Celtic itakuwa na safari ndefu hadi Urusi baada ya kikosi cha Brendan Rodgers kupangiwa Zenit St Petersburg ya Roberto Mancini.

  Arsenal itamenyana na Ostersunds ya Sweden inayomilikiwa na Muingereza, Graham Potter katika hatua ya 32 ya Europa League PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Nayo Lyon, wenyeji wa fainali itakayopigwa Mei 16 mwakani, watamenyana na Villarreal na mchezo mwingine utazikutanisha Leipzig na Napoli.
  Kocha Gennaro Gattuso wa AC Milan amepewa Ludugorets ya Bulgaria. 
  Mechi za kwanza zitachezewa Februari 15 na marudiano yatakuwa Februari 22, mwaka 2018. 

  RATIBA 32 BORA EUROPA LEAGUE 

  Borussia Dortmund vs Atalanta
  Nice vs Lokomotiv Moscow
  Copenhagen vs Atletico Madrid
  Spartak Moscow vs Athletic Bilbao
  AEK Athens vs Dynamo Kiev
  Celtic vs Zenit St Petersburg
  Napoli vs Leipzig
  Red Star Belgrade vs CSKA Moscow
  Lyon vs Villarreal
  Real Sociedad vs Salzbug
  Partizan Belgrade vs Viktoria Plzen
  Steaua Bucharest vs Lazio
  Ludogorets vs AC Milan
  Astana vs Sporting Lisbon
  Ostersunds vs Arsenal
  Marseille vs Braga 
   
  Mechi za kwanza zitachezwa Februari 15 na marudiano yatakuwa Februari 22 mwaka 2018 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAPELEKWA SWEDEN 32 BORA EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top