• HABARI MPYA

  Friday, December 08, 2017

  AHMAD AAHIDI KUWAPA NAFASI ZAIDI WANASOKA WASTAAFU CAF

  RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad ametilia mkazo mpango wake ya kuwatumia wanasoka wastaafu katika uongozi wake kuliletea maendeleo bara hili.
  Anawachukuliwa wanasoka kama wahusika wakuu wa mchezo, ambao ni muhimu kujumuishwa kutokana na utaalamu na uzoefu wake.
  “Tangu kuchaguliwa kwangu nchini Ethiopia mwezi Machi mwaka huu, shirikisho letu limewapa wanasoka nafasi kubwa kwa kuwakaribisha magwiji ambao waliweka historia kwenye soka ya Afrika katika mkutano uliofanyika nchini Morocco kutazama dira yetu ya soka barani,” amesema Ahmad wakati wakati wa mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Kimataifa Wanasoka wa Kulipwa (FIFPro) jumatano mjini Cairo, Misri.
  Rais wa CAF, Ahmad (kulia) wakati mkutano Mkuu wa FIFPro juzi mjini Cairo, Misri

  Ameihakikishia FIFPro ushirikiano kutoka CAF na kusaidia kuboresha maslahi na hali za maisha ya wachezaji wa Afrika kwa ujumla, ambao wanacheza barani hapa.
  “Moja kati ya mapambano ya kwanza ambayo itabidi tuunganishe nguvu zetu na nyinyi (FIFPro) itakuwa ni malipo ya mishahara wachezaji wanaosajiliwa na klabu za Afrika. Ilivyo, asilimia 55 ya wachezaji katika bara letu wanachelewa kulipwa, au hawalipwi kabisa,”amesema Hamad.
  “Tunajaribu kufanya kila jitihada kuhakikisha klabu zote zinazocheza michuano ya Afrika zipo katika msimamo mzuri na wachezaji ilionao wana mikataba. Tutaziagiza Kamati zetu kuangalia namna zote na njia zote, ambazo wanasoka wetu wanaweza kufanya kazi katika mazingira salama wakilipwa mishahara na stahiki zao zote,”.
  Mkutano huo Mkuu wa siku tatu ulimalizika Alhamisi ya Desemba 7 na ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka madaraja tofauti ya FIFPro – mabara ya Afrika, Amerika, Asia/Oceania na Ulaya.
  Ikiwa ilianzishwa mwaka 1965, lengo kuu la FIFPro kuviunganishsa pamoja vyama vyote vya wachezaji duniani, bila kujali nchi zao, dini, itikadi za siasa, harakati au jinsi ili kuimarisha umoja na mshikamano baina ya wachezaji.
  Katika Mkutano wa mwaka huu, kiungo wa zamani wa Cameroon, Geremi Njitap alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa bodi na Mfaransa, Philippe Piat alichaguliwa tena kuwa Rais kwa miaka mingine minne.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AHMAD AAHIDI KUWAPA NAFASI ZAIDI WANASOKA WASTAAFU CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top