• HABARI MPYA

  Thursday, November 16, 2017

  STARS KUANZA NA LIBYA KOMBE LA CHALLENGE, IPO KUNDI MOJA NA KENYA, RWANDA, ZANZIBAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi A katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge pamoja na ndugu zao, Zanzibar, wenyeji Kenya, Rwanda na waalikwa Libya.
  Katika droo iliyopangwa leo mjini Nairobi, Kenya ambako michuano hiyo inafanyika kuanzia Desemba 3 hadi 17, mwaka huu, Kundi B lina timu za Uganda, Zimbabwe, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.
  Kilimanjaro Stars itafungua dimba na Libya Desemba 3, mwaka huu mchezo ambao utafuatiwa na mechi kati ya wenyeji, Kenya dhidi ya Rwanda.
  Kilimanjaro Stars itafungua dimba na Libya Desemba 3, mwaka huu kwenye Kombe la CECAFA Challenge

  Kili Stars itarudi uwanjani Desemba 7 kumenyana na Zanzibar Heroes, Desemba 9  na Rwanda kabla ya kumaliza mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na wenyeji, Kenya Desemba 11.
  Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Desemba 12 na Nusu Fainali zitachezwa Desemba 14 na 15, wakati Desemba 16 itachezwa mechi ya kusaka mshindi wa tatu ikifuatiwa na fainali.
  CECAFA Challenge ndiyo michuano mikongwe zaidi ya soka barani Afrika ambayo ilianza mwaka 1926 ikijulikana kama Kombe la Gossage hadi mwaka 1966, ilipobadilishwa na kuwa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati hadi mwaka 1971 ilipobadilishwa tena na kuwa CECAFA Challenge.
  Wadhamini tofauti wamekuwa wakiingia na kutoka kwa kipindi chote hicho, lakini taarifa zinasema kuanzia mwaka huu Televisheni namba moja Afrika Mashariki na Kati, Azam TV ndiyo wanakuwa wadhamini wapya ambao pia watakuwa wanarusha moja kwa moja michuano hiyo. 
  Uganda ndiyo mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo tangu mwaka 1971, wakiwa wamelitwaa mara 14, wakifuatiwa na Kenya mara sita, Ethiopia mara nne na Tanzania mara tatu.
  Uganda, The Cranes pia ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa taji la michuano hiyo mwaka 2015 nchini Ethiopia wakiwafunga Rwanda 1-0 kwenye fainali mjini Addis Ababa, wakati mwaka jana michuano hiyo haikufanyika kwa sababu ya kukosa nchi mwenyeji.  

  RATIBA CHALENGE 2017
  Desemba 3, 2017
  Libya vs Tanzania
  Kenya vs Rwanda
  Desemba 4, 2017
  Burundi vs Ethiopia
  Uganda vs Zimbabwe
  Desemba 5, 2017
  Zanzibar vs Rwanda
  Kenya vs Libya
  Desemba 6, 2017
  Sudan Kusini vs Zimbabwe
  Uganda vs Burundi
  Desemba 7, 2017
  Tanzania vs Zanzibar
  Rwanda vs Libya
  Desemba 8, 2017
  Sudan Kusini vs Ethiopia
  Zimbabwe vs Burundi
  Desemba 9, 2017
  Rwanda vs Tanzania
  Kenya vs Zanzibar
  Desemba 10, 2017
  Sudan Kusini vs Burundi
  Ethiopia vs Uganda
  Desemba 11, 2017
  Libya vs Zanzibar
  Kenya vs Tanzania
  Desemba 12, 2017
  Uganda vs Sudan Kusini
  Zimbabwe vs Ethiopia
  Desemba 13, 2017
  MAPUMZIKO
  Desemba 14, 2017
  NUSU FAINALI
  Mshindi Kundi A Vs Mshindi wa Pili Kundi B
  Desemba 15, 2017
  Mshindi Kundi B Vs Mshindi wa Pili Kundi A
  Desemba 16, 2017
  MAPUMZIKO
  Desemba 17, 2017
  Fainali/Mshindi wa Tatu
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STARS KUANZA NA LIBYA KOMBE LA CHALLENGE, IPO KUNDI MOJA NA KENYA, RWANDA, ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top