• HABARI MPYA

  Sunday, November 19, 2017

  SIMEONE ASEMA GRIEZMANN ANAWEZA KUONDOKA ATLETIO

  KOCHA Diego Simeone amedokeza kwamba Antoine Griezmann anayetakiwa na Manchester Unitedanaweza kuondoka Atletico Madrid.
  Simeone amesema hayo baada ya kuulizwa mustakabali wa Griezmann kufuatia kuzomewa wakati Atletico Madrid ikilazimishwa sare ya 0-0 na Real Madrid jana katika La Liga.
  Kocha huyo wa Atletico alimpumzisha mshambuliaji wake huyo Mfaransa kwa mara ya pili mfululizo kwenye mechi ya ligi na akazomewa kipindi cha pili wakati anakwenda benchi.
  Simeone alisema: "Nyumbani nilifundishwa kwamba wakati mmoja wenu anapokuwa sehemu ya familia unapaswa kuwasimamia hadi kifo,".

  Diego Simeone amesema Antoine Griezmann anayetakiwa na Manchester United, anaweza kuondoka Atletico Madrid 


  Na kwa sababu mashabiki wa Atletico Madrid wamekwishaanza kuhisi siki za Griezmann zinahesabika kutokana na kutakiwa na United waliokaribia kumsajili msimu huu na Barcelona wanamtaka pia kwa mwakani.
  Griezmann amefunga mabao mawili tu msimu huu katika mechi 10 alizocheza na Simeone amerudia mara mbili kusema katika mkutano na Waandishi wa Habari. 
  "Unamsapoti mtu hadi kifo hadi atakapokuwa si sehemu ya familia yako tena,".
  Kiungo Saul amesema: "People wanatakiwa kumtetea. Greizman ni mchezaji wetu muhimu na tunatakiwa kumsapoti wakati wote,".
  Dau la kumnunua Griezmann lilikuwa Euro Milioni 200 January mwaka huu, lakini litapungua hadi Milioni 100 msimu ujao.
  Manchester United ilikaribia kumsajili msimu huu, lakini ikashindwa kutokana na Atletico Madrid kufungiwa kusajli mchezaji mpya hadi mwaka 2018.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMEONE ASEMA GRIEZMANN ANAWEZA KUONDOKA ATLETIO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top