• HABARI MPYA

  Saturday, November 11, 2017

  SIMBA YAWATUMIA SALAMU TANZANIA PRISONS…YASHINDA 3-1 SUMBAWANGA

  Na Mwandishi Wetu, SUMBAWANGA
  TIMU ya Simba SC leo imepeleka salamu kwa Tanzania Prisons, baada ya kuichapa Kaengesa ya Sumbawanga mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Nelson Mandela mjini hapa.
  Simba itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Novemba 18, Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Na katika kujiandaa na mchezo huo, Simba iliweka kambi fupi Sumbawanga tangu Jumatano, ikitokea Mpanda mkoani Katavi ambako Jumanne ilicheza mechi na wenyeji, Nyundo FC na kutoka sare ya 0-0.
  Juma Luizio (kulia) na Mohammed 'Mo' Ibrahim wote wamefunga leo Simba ikishinda 3-1 Sumbawanga PICHA YA MAKTABA

  Lakini katika mchezo wa leo, Simba imewapa onyo mahasimu wao wajao katika Ligi Kuu baada ya kuichapa Kaengesa 3-1.
  Mabao ya Simba yamefungwa na kiungo Mohammed ‘Mo’ Ibrahim moja dakika ya 29 na mshambuliaji Juma Luizo mawili dakika ya 47 na 92.
  Simba itaondoka hapa kesho kwenda Mbeya kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya Prisons. 
  Kikosi cha Simba leo kilikuwa; Emmanuel Mseja/Ali Salim dk70, Ally Shomary, Jamal Mwambeleko/Nicholas Gyan dk60, James Kotei, Yussuf Mlipili, Mwinyo Kazimoto, Jamal Mnyate, Muzamil Yassin, Joma Luizo, Haruna Niyonzima na Mo Ibrahim. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAWATUMIA SALAMU TANZANIA PRISONS…YASHINDA 3-1 SUMBAWANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top