• HABARI MPYA

    Tuesday, November 14, 2017

    SAMATTA AANZA MAZOEZI MEPESI YA GYM UBELGIJI

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    SIKU nne baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa goti, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo ameanza maozezi mepesi ya gym.
    Akizunguma na Bin Zubeiry Sports – Online leo kutoka Genk, Samatta amesema kwamba leo ameanza maozezi mepesi ya gym.
    “Nimeanza mazoezi mepesi ya gym leo kwa maelekezo ya Daktari. Ni taratibu tu ili kujiweka vizuri, nikitoka hapa natembele fimbo kama kawaida,”amesema Samatta aliyefanyiwa upasuaji wa goti hilo Novemba 10 mjini Genk, Ubelgiji.
    Mbwana Samatta akifanya mazoezi mepesi ya gym baada ya kufanyiwa upasuaji Novemba 10
    Na akitoka gym, Mbwana Samatta hutumia fimbo maalum kutembea

    Samatta yuko katika wiki ya kwanza kati ya sita za mapumziko kufuatia kuumia Novemba 4, mwaka huu akiichezea klabu yake, KRC ikilazimishwa sare ya 0-0 Jumamosi na Lokeren katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
    Na baada ya kufanyiwa vipimo ikagundulika Samatta ameumia kwenye mishipa midogo ya goti lake la mguu wa kulia ambayo ilichanika, hivyo kuhitaji kufanyiwa upasuaji mdogo ili apone sawia.
    Samatta aliumia akiichezea mechi ya 70 Genk tangu alipojiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Na katika mechi hizo 70, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA AANZA MAZOEZI MEPESI YA GYM UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top