• HABARI MPYA

  Monday, November 13, 2017

  RONALDO SASA NI 'BABA WANNE', MPENZI WAKE AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE

  MWANASOKA nyota, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ya Hispania, amesherehekea kuzaliwa kwa mtoto wake wa nne.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ameposti picha ya mchumba wake, Georgina Rodriquez, mwenye umri wa miaka 22, akiwa amemshika mtoto wao pembeni yake wakiwa na mtoto wake mkubwa, Cristiano Jr. 
  Ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram: "Alana Martina amejifungua! Wote Geo na Alana wanaendelea vizuri! Wote tuna furaha sana!" 
  Familia iliwasili katika hospitali ya Quiron Universal mjini Madrid, jirani na nyumbani kwa mwanasoka huyo eneo la watu mashuhuri, La Finca, mapema Jumapili.
  Ilifikiriwa mtoto wake wa nne angezaliwa siku moja na mtoto wake wa kwanza, Novemba 21, lakini Jumapili jioni Ronaldo alithibitisha wote walikuwa wako vizuri.
  Cristiano Ronaldo na mpenzi wake, Georgina Rodriguez wamepata mtoto wa kike 

  Georgina, ambaye nusu ni Mspaniola na nusu Muargentina, mwezi Agosti alisema namna anavyojiandaa kupata mtoto Alana Martina wakati anakula Mediterranean.
  Wiki iliyopita, Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano alisema kuwa baba ni uzoefu mzuri, baada ya kupanua familia yake  mwezi Juni kufuatia kuzaliwa kwa mapacha Eva na Mateo nchini Marekani na kurejea nao Madrid, ambako wanaishi na mama yao wa kambo.
  Cristiano Jr, mwenye umri wa miaka saba, pia anafikiriwa kuzaliwa na mama asiyejulikana nchini Marekani.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO SASA NI 'BABA WANNE', MPENZI WAKE AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top