• HABARI MPYA

  Thursday, November 16, 2017

  PROFESA KAPUYA ATUA YANGA, AKABIDHIWA KOMBE LA UBINGWA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAZIRI wa zamani wa Michezo nchini, Profesa Juma Othman Kapuya leo amevunja mwiko na kuzuru makao makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani mjini Dar es Salaam.
  Kapuya ambaye ni mpenzi na mwanachama wa klabu ya Simba, ambao ni mahasimu wa Yanga, alifika Jangwani pamoja na jamaa zake kutoka Kaliua, mkoani Tabora. 
  Jamaa hao walisema Waziri kapuya alikwenda kuwatembeza makao makuu ya klabu ya Simba, Mtaa wa Msimbazi, wakati wao ni wapenzi wa Yanga, hivyo wakamshinikiza awafikishe Jangwani.
  Waziri wa zamani wa Michezo nchini, Profesa Juma Kapuya akiwa makao makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani leo mjini Dar es Salaam

  Walipofika Jangwani, walipokewa na Katibu Mkuu wa klabu, Charles Boniface Mkwasa ambaye alimshikisha Waziri Kapuya Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambalo mara ya mwisho walilitwaa mwaka 2012.
  Pamoja na hayo, Waziri Kapuya alipata fursa ya kukagua jengo na ofisi mbalimbali za klabu na kupongeza kwa baadhi ya mambo yaliyomvutia.  

  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PROFESA KAPUYA ATUA YANGA, AKABIDHIWA KOMBE LA UBINGWA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top