• HABARI MPYA

    Sunday, November 12, 2017

    MOROCCO WAFUZU KOMBE LA DUNIA, IVORY COAST WAKOSA SAFARI

    TIMU ya taifa ya Morocco imekata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi baada ya kuwapiga wenyeji, Ivory Coast mabao 2-0 mjini Abidjan.
    Simba wa Atlas waliingia kwenye mechi hiyo Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny wakiwa wanawazidi pointi moja Tembo wa Ivory Coast na walihitaji sare tu ili kupata nafasi ya kwenda Urusi mwakani.
    Hata hivyo, mabao mawili ndani ya dakika tano kutoka kwa Nabil Dirar na Medhi Benatia yaliwapa ushindi mzuri katika mechi hiyo ya Kundi C.

    Wachezaji wa Morocco wakishangilia baada ya ushindi wao wa jana unaowawezesha kufuzu Kombe la Dunia
     PICHA ZAIDI GONGA HAPA 



    TIMU ZILIZOFUZU KOMBE LA DUNIA URUDI 2018 HADI SASA

    Urusi, Brazil, Uruguay, Argentina, Colombia, Mexico, Costa Rica, Panama, Iran, 
    Korea Kusini, Japan, Saudi Arabia, Nigeria, Misri, Senegal, Morocco, Tunisia, Ubelgiji, Ujerumani, England, Hispania, Poland, Iceland, Serbia, Ureno na Ufaransa
    Timu ambazo bado hazijafuzu...
    Peru/New Zealand
    Honduras/Australia
    Northern Ireland/Switzerland
    Croatia/Ugiriki
    Sweden/Italia
    Denmark/Ireland 
    Winga wa Fenerbahce, Dirar aliifungia Morocco bao la kwanza dakika ya 25 baada ya krosi yake kutoka upande wa kulia kuingia moja kwa moja kwenye nyavu za Ivory Coast.
    Nahodha Medhi Benatia akafunga bao la pili kiulaini dakika ya 30.
    Ivory Coast ilpata nafasi kadhaa za kufunga mabao, lakini ikashindwa kuzitumia vizuri ikiwemo ya beki wa Tottenham, Serge Aurier aliyepiga juu ya lango kipindi cha pili. 
    Matokeo hayo yanaifanya timu ya Marc Wilmots, Ivory Coast ikose fainali za Kombe la Dunia mwakani, maana yake majina makubwa ya nyota wa timu hiyo wanaocheza Ligi Kuu ya England kama Wilfried Zaha, Serge Aurier na Eric Bailly yatakakuwa mapumzikoni katikati ya mwakani.
    Morocco inaungana na Tunisia kukamilisha nchi tano za Afrika zilizofuzu Kombe la Dunia, nyingine zikiwa ni Nigeria, Misri na Senegal.
    Ushindi huom, unamfanya kocha Herve Renard awaumize waajiri wake wa zamani, timu ambayo aliiongoza kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015.
    Morocco imefuzu siyo tu bila kupoteza mechi, ikishinda mechi tatu na kutoa sare tatu, pia imeruhusu nyavu zake kutikisika mara moja tu.
    Renard anasaidiwa na Mwanasoka Bora wa zamani wa Afrika, Mustapha Hadji, kiungo wa zamani wa Morocco na klabu za Coventry na Aston Villa.
    Kikosi cha Ivory Coast kilikuwa: Gbohouo, Aurier, Gbamin, Kanon, Deli/Konan dk45, Fofana/Cornet dk62, Gradel, Kessie, Zaha, Doumbia na Gervinho/Kalou dk76.
    Morocco: Mohamedi, Dirar, Benatia, Saiss, Hakimi, Boussoufa, El Ahmadi, Belhanda/Fajr dk90+1, Ziyech/S Amrabat dk82, Boutaib/Bencharki dk75 na N Amrabat.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOROCCO WAFUZU KOMBE LA DUNIA, IVORY COAST WAKOSA SAFARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top